Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) Nehemia Mchechu (mwenye kofia) wakiangalia jengo la Jengo la Hospitali ya Rufaa ya Mwalimu Nyerere Memorial Medical Center iliyopo eneo la Kwangwa Manispaa ya Musoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) Nehemia Mchechu akizungumza na wadau wa Shirika hilo katika ukumbi wa uwekezaji wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara juu ya ujenzi wa nyumba za shirika hiloManispaa ya Musoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) Nehemia Mchechu (mwenye kofia) akiwa na watendaji wengine wa shirika hilo na serikali wakielekea kwenye jengo la Jengo la Hospitali ya Rufaa ya Mwalimu Nyerere Memorial Medical Center iliyopo eneo la Kwangwa Manispaa ya Musoma.
Na Thomas Dominick,
Musoma
WAKAZI wa Buhare Manispaa ya
Musoma wapo mbioni kulipwa fidia kutoka kwenye Shirika la Nyumba Tanzania (NHC)
kwa ajili ya kupisha ujenzi wa mji mpya wa Musoma.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi
mtendaji wa Shirika hilo, Nehemia Mchechu ambaye alikuwa na ziara ya kutembelea
mkoa huo aliwatoa wasiwasi viongozi wa Manispaa hiyo kuhusiana na uendelezaji
wa mji huo baada ya kuwapatie eneo hilo tangu mwaka 2010.
Nehemia alisema kuwa shirika
hilo linatarajia kutoa fidia hiyo mwezi mei mwaka huu baada ya kukamilisha
taratibu zote za kufanya tathimini ya nyumba
na maeneo ya wakazi wa eneo hilo.
“taratibu zote za kuwalipa
fidia zimekamilika na mwezi ujao (mei) tutaanza kutoa malipo ya fidia kwa
wakazi hao ili wapishe ujenzi huo ambao tunatarajia kuanza katika kipindi cha
fedha cha mwaka 2013/14,”alisema Mchechu.
Alisema kuwa eneo hilo
litatumika kujengwa nyumba za kisasa ambazo zitakuwa kwa ajili ya kupangisha
pamoja na kuuza kwa wananchi kwa bei nafuu na kupata makazi bora.
Mchechu alisema kuwa pamoja
na eneo hilo la Buhare pia watajenga nyumba zingine katika wilaya za Serengeti
na wilaya mpya Butiama kwa ajili ya kumuenzi baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere
kwani ndiye mwazilishi wa shirika hilo.
“Pamoja na Buhare lakini
tunatarajia kufanya ujenzi katika wilaya mbili ya Serengeti na Butiama na
Butiama ni kwa ajili ya kumuenzi baba wa Taifa kwani ndiye mwanzilishi wa
shirika letu lazima tumrudishie heshima yake,”alisema.
Naye Naibu Meya Bwire
Nyamwero alimtaka Mkurugenzi huyo kufanya zoezi hilo bila kuchelewa kwani
wananchi wa Musoma wanasubiria kwa hamu mradi huo na kumuhakikishia kuwa kama
anataka eneo jingine atapewa.
“Napenda kumtoa wasiwasi
mkurugenzi wa NHC kuwa tupo tayari kupokea mradi huo mkubwa lakini
nimuhakikishie kuwa kama anataka eneo jingine aseme tutampatia,”alisema
Nyamwero.
Mkuu wa Mkoa John Tuppa
alisema kuwa mkoa wa Mara kuna maeneo mengi na makubwa kwa ajili ya uwekezaji
hivyo watumie fursa ya Shirika hilo kuwekeza kwa manufaa ya wananchi wao.
M WISHO