MKURUGENZI MPYA WA HALMASHAURI YA BUTIAMA RICHARD MIHAYO AKIWA PAMOJA NA HATI YA UANZISHWAJI KWA HALMASHAURI HIYO.
Na Thomas Dominick
Butiama
WANANCHI wa Tarafa ya
Kiagata Wilaya ya Butiama, Mkoa wa Mara wameiomba Serikali
kuipatia Kata hiyo jimbo linalojitegemea
kutokana na jimbo la Musoma Vijijini linalotawaliwa na
Mbunge Nimrod Mkono kuwa kubwa na
kushindwa kufikisha huduma muhimu kwa wananchi.
Akitoa hoja hiyo
katika kikao maalum cha uvuvunjaji wa Halmashauri hiyo na kuzaa
Halmashauri mpya ya Butiama, Diwani wa Kata ya Buswahili, Tarafa ya
Kiagata Kawaki Marwa alisema kuwa
kutokana na ukubwa wa eneo hilo
imekuwa vigumu kuwafikishia huduma muhimu kwa wakazi wa maeneo hayo
kufika.
“Mheshimiwa
Mwenyekiti eneo la Kiagata ni kubwa sana, tunaomba sisi kama wananchi wa
maeneo hayo Serikali ilikate jimbo hilo na tuwe na majimbo mawili ili
kuweza kuwafikishia huduma wananchi kirahisi kuliko ilivyokuwa
sasa,”alisema Marwa
Alisema kuwa Tarafa
hiyo ina kata nne na wakazi 35,274 kwa takwimu za sensa iliyofanyika
mwaka 2012, nchi mzima kitu ambacho kimesababisha huduma zinazotolewa
na mbunge huyo kuwa zinawanufaisha wananchi wa upande mmoja na
upande mwingine kuteseka.
Naye Mkuu wa Mkoa huo
John Tuppa wakati akitoa hotuba kabla
ajakadhidhi hati ya
kuashiria uanzishwaji wa Halmashauri hiyo mpya ya Butiama kwa Kaimu
Mkurugenzi Richard Mihayo alisema kuwa Halmashauri ya Musoma ina eneo
kubwa hivyo inahitaji kupata majimbo mengine mawili.
“Changamoto
zilizokuwa zinaikabili Halmashauri hii ni ukubwa wa eneo na hapa tumeanza tu
kugawa katika Halmashauri mbili lakini inatakiwa iwe na majimbo aidha
matatu ya uchaguzi ili kuweza kuwaqfikishia huduma wananchi wa
maeneo hao,” alisema Tuppa.
Alisema kuwa pamoja
na hilo viongozi wa Halmashauri hizo waache utendaji kazi wa
mazoea ili waweze kuwatendea haki wananchi wao ikiwa pamoja na kuwatatulia
kero mbalimbali zinazowakabili.
Ugawaji wa
Halmashauri hizo ilifanyika ikiwa ni pamoja na kugawana raslimali na madeni
yaliyokuwepo katika Halmashauri hiyo hatua hiyo ambayo ilikwisha kwa
amani na utulivu huku kila mjumbe akiridhia ugawaji huo.
Hivi karibuni katika
mchakato kama huo wa kugawa Halmashauri ya Tarime na Halmashauri ya Mji
wa Tarime vurugu zilitokea kutokana na madiwani watatu wa viti
maalumu wa CCM na Chadema kukataliwa kuingiwa Mjini kwa madai hawakai maeneo
ya mjini na kusababisha kutoelewana na madiwani kurushia maneno na
kuvunjiaka bila muafa.
MWISHO
Na Thomas Dominick
Butiama.
HALMASHARI ya Wilaya
ya Musoma Mkoa wa Mara imejikuta katika wakati mgumu pale baada ya
madiwani kuitaka halmashauri kutoa ufafanuzi wa kina juu ya
malimbikizo ya madeni kubwa la Milioni 402 ambazo zimeweza kusababisha kuzorota
kwa suala zima la Maendeleo kwa
wananchi.
Wakichangia hoja
mbalimbali hii leo katika kikao maalum
kilichokuwa na lengo la kujadili
mgawanyiko wa rasirimali kati ya halmashauri ya wilayaya Musoma pamoja na Butiama, Diwani wa kata ya
Nyambono Grayson Mfungo
amesema kuwa malimbikizo ya milioni 402
ni mzigo mkubwa kwa
Halmashauri kitendo ambacho kinaweza kukwamisha baadhi ya shuguli za
kimaendeleo.
Kambi ya upinzani
walitaka kujua halmashauri ilikuwa wapi mpaka
inafikia hatua ya
malimbikizo kwa watendaji wanaokaimu
idara mbali mbali na kudai kuwa
watakubaliana na mgawanyiko wa raslimali
endapo tu halmashauri itatoa
majibu ya kuridhisha kuhusiana na suala hili.
Akijibu hoja hiyo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Musoma Fidelica Myovela,
alikiri kuwa halmashauri inakabiliwa na
deni kubwa na sehemu kubwa ya
deni hilo nikutokana na posho za kukaimu nafasi ya Ukuu wa Idara ambapo zilistahili kulipwa kwa wakuu
mbalimbali wa idara.
Naye Mkuu wa Mkoa wa
huo, John Tuppa alikiri kupokea taarifa za malimbikizo ya madeni
na amehaidi kulipeleka suala hilo katika
serikari kuu sambamba
na uwasilishwaji wa wakuu mbali mbali wa idara ili kuweza kuondokana
na tatizo la ukaimu ambapo limekuwa
likisababisha mzigo
mkubwa Kwa halmashauri.
Aidha alizitaka
halmashauri kuhakikisha kuwa
zinaboresha mapato yake ya ndani na kuziba
mianya yote inayopita fedha hizo katika mifuko ya watu binafsi ili kuepuka ongezeko la msaada wa kifedha kutoka serikali kuu.
“Viongozi wanashindwa
kusimamia sheria za ukusanyaji mapato na hicho ndicho chanzo cha
upotevu wa mapato ya ndani utakuta viongozi wana vitabu bandia vya
risti za kukusanyia fedha za serikali, viongozi kama hawa
hawatufai,”alisema Tuppa.
Halmashauri ya wilaya
ya Musoma imeweza kujitenga rasmi na kuzaa wilaya mbili Butiama pamoja na Musoma Vijijini inayopigiwa
debe iitwe kwa jina Nyanja lengo
kuu likiwa kurahisisha huduma kwa wananchi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment