Thursday, April 25, 2013

KIJANA MMOJA AFANYA MAPENZI NA KUKU MANISPAA YA MUSOMA MKOA WA MARA

* Ashiliwa na Polisi
* Kuku apelekwa kwa Afisa Mifugo kwa uchunguzi
* Tukio jingine mama amchoma wifi yake moto mdomoni na
    sehemu za siri
* Wananchi wampa kichapo alazwa Hospitali ya Mkoa wa Mara.


 Makamanda wa Polisi wakiwa katika mkutano wa waandishi wa habari ( hawapo Pichani) katika ofisi ya  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya kijana aliyefanya mapenzi na kuku.
Huyu ndiye kuku aliyefanyiwa unyama na kijana Yusuph Bakari ambaye alifanya naye mapenzi chumbani kwake katika mtaa wa Kigera manispaa ya Musoma na kumsababishia maumivu makali.



Na Thomas Dominick,
Musoma


KIJANA aliyejulikana kwa jina la Yusuph Bakari (28) Mkazi wa kigera
manispaa ya Musoma Mkoa wa Mara anashikiliwa na Polisi kwa Kosa la
kufanya mapenzi na kuku jike na kumsababishia maumivu makali.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana kamanda wa
Polisi mkoa Absalom Mwakyoma alisema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili
24 Mwaka huu saa 3 asubuhi.

Mwakyoma alisema kuwa kuku huyo alikuwa wa Nyamera Kitambara (26)
ambaye ni mmiliki wa nyumba ambayo amepanga Bakari baada ya tukio hilo
mama huyo alikerwa na kuchukua hatua ya kupiga yowe na wananchi kwenda
kumsaidia kumkamata kijana huyo na kumfikisha kituo cha polisi.

Kutokana na maumivu makali aliyemsababishia kuku huyo alipeolekwa kwa
Afisa mifugo kwa ajili ya uchunguzi.

Wakati huo huo, mama mmoja Elizabeth Bureko (26) Mkazi wa Nyamatare
Manispaa ya Musoma amelazwa katika Hosspitali ya Mkoa wa Mara baada ya
kupokea kichapo toka kwa wananchi wenye hasira kwa sababu ya kumchoma
kwa moto wa kibari mdomoni na sehemu za siri wifi yake aliyetambulika
kwa jina la Rhobi Marwa (8).

Kamanda Mwakyoma alisema tukio hilo lililotokea Aprili 24 mwaka huu
ambapo chanzo chake ni mama huyo alimkuta wifi yake huyo akimpatia uji
mtoto wake mwenye miezi miwili huku akilia na kumshutumu kuwa uji huo
alikuwa ana kunywa yeye badala ya kumpa mtoto.

"Wananchi baada ya kuona kitendo hicho walikerwa na kuanza kumpatia
kichapo mama huyo na kwa sasa amelazwa hospitalini kwa matibabu na
akishapona sharia itachukua mkondo wake,"alisema mwakyoma.

Mwakyoma ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za uhalifu ambao
unaweza kutokea na umeshatokea ili kuweka Mkoa huo katika hali ya
amani na usalama.

MWISHO
Read More...

Sunday, April 21, 2013

PSPF YAWAJENGEA UELEWA WA MFUKO HUO WANACHUO WA CHUO CHA UALIMU BUNDA HIVI KARIBUNI



 *Wanachuo hao wataka umri wa kustaafu ushuke hadi miaka 40
*PSPF yajenga nyumba kwa ajili ya kuwakopesha wanachama wao
*Vijana wapendelewa zaidi na mfuko huo


Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma Sudi Hamza akiandika fomula ya kupata mafao kwa wanachuo wa chuo cha ualimu Bunda wanaotarajia kuanza mitihani yao mei 6 mwaka huu na kupata ajira ya Serikali
 Wanachuo wa chuo cha Ualimu Bunda wakimsikiliza kwa makini Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma Sudi Hamza katika semina ya siku moja chuoni hapo.
 Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma Sudi Hamza akiwaelezea wanachuo wa chuo cha Bunda umuhimu wa kujiunga na mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma na mafao ambayo wanaweza kupata wakiwa wananchama wa mfuko huo.
 Wanachuo wa Chuo cha Ualimu Bunda wakipata soda baada ya kumalizikia semina ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma PSPF iliyofanyika chuoni hapo ili kuwajengea uwezo wa kuufahamu vizuri mfuko huo..


 Wanachuo wakisoma vipeperushi vya Mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa Umma (PSPF) katika semina ya siku moja iliyofanyika chuoni hapo.


 Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa Umma (PSPF) Mkoa wa Mara Sudi Hamza akitoa formula  kwa wanachuo wa Chuo cha Ualimu Bunda jinsi ya kupata mafao yako ya uzee baada ya kustaafu.
 Wanachuo wa chuo cha Ualimu bunda wakimsikiliza Afisa Mfawidhi wa PSPF Sudi Hamza wakati wa semina ya siku moja kwa ajili ya kuwajengea uwezo na uelewa wa mfuko huo.

Na Thomas Dominick,
Bunda

MFUKO wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) umewajengea uwezo na ufahamu wa mfuko huo wa Pensheni wanachuo wa Chuo cha Ualimu Bunda kilichopo wilaya ya Bunda Mkoani Mara wanaotarajia kuajiriwa na Serikali mwaka huu.

Akitoa semina ya siku moja chuoni hapo Afisa Mfawidhi wa PSPF  Mkoa wa huo, Sudi Hamza aliwataka wanachuo hao wanaotarajia kuanza mitihani ya mwisho mei 6 mwaka huu kuwa makini na mifuko hiyo pindi watakapoajiri na Serikali.

“Nimekuja chuoni hapa kwa ajili ya kufanya semina na ninyi ili kuwapatia ufahamu wa na kuwaongezea uwezo wa kuutambua vizuri mfuko wa PSPF na kujua faida ya kujiunga nao kwani ndio unaotoa faida kubwa kwa wanachama wake,”alisema Hamza.

Baada ya Hamza kuwasilisha mada juu ya mfuko huo wanachuo hao walipewa nafasi ya kuuliza maswali na mapendekezo mbalimbali ambayo yangeweza kuwajenga zaidi.

Ambapo mwanchuo aliyejulikana kwa jina la Kinguye Wambura aliiomba PSPF kwa kushirikiana na Serikali kujadili kwa kina juu ya umri wa kustaafu kwa watumishi kutoka miaka 55 ya hiari na 60 ya lazima hadi kufikia 40 hadi 45.

“Hii hali ya kusubiria hadi miaka 55 na 60 ni ni uonevu kwa watumishi kwani hadi kufikia umri huo mtumishi anakuwa hana nguvu ya kufanya biashara na akili inakuwa imechoka haitamnufaisha fedha hiyo kwani akili inakuwa imechoka hivyo Serikali ipunguze miaka hadi 40 na 45 ya lazima,” alisema Wambura.

Naye mwanachuo aliyejitambulisha kwa jina la Agnes Ezekiel alimuuliza Afisa huyo kuwa kama kuna uwezo wa kujiunga na mifuko zaidi ya mmoja kwa ajili ya kupata mafao mengi pindi atakapostaafu.

Hamza alimjibu  kuwa hiyo haiwezekani kujiunga na mfuko zaidi ya mmoja labda ajiunge na Mfuko wa Hiari uliopo chini ya PSPF ambapo atalipwa mafao yake baada ya kuwekeza ambapo fedha hiyo isipungue sh. 10,000/= kwa mwezi.

Alisema kuwa pia PSPF inatoa mafao ya Elimu ambapo kama mwanachama anataka kwenda kusoma yeye ama motto wake unampatia fedha hizo kwa ajili ya kulipia ada, aliongeza kuwa PSPF inatoa mafao ya ujasiriamali kwa mwanachama ambaye anataka kuanzisha biashara.

Pia alisema kuwa PSPF inajenga nyumba sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuwakopesha wanachama wake waliotimiza miaka mitano ili kuwakwamua kimaisha ambapo mwanachama atatakiwa kulipa ndani ya miaka 25.

“Kutokana na kujua ugumu wa maisha tumeamua kujikita katika kujenga nyumba bora za kisasa kwa ajili ya kuwakopesha wanachama wetu ambazo watalipa ndani ya mika 25 na sharti kuu lazima atomize miaka mitano kazini,”alisema.

Hamza aliwatoa wasiwasi wanachuo kuwa serikali imeweka ofisi kila mkoa kwa ajili ya kupunguza usumbufu kwa wanachama wao kusafiri kufuatilia mafao yao Makao Makuu Dar es Salaam na kufuata ushauri na maelekezo mbalimbali.

Kwa sasa mtumishi akiwa na shida hana haja ya kwenda Makao Makuu ya PSPF anachotakiwa ni kwenda makao makuu ya Mkoa kwani kila mkoa kuna ofisi yetu kwa ajili ya ushauri na kama una tatizo linamalizikia hapo tena bila usumbufu wowote,”alisema.

PSPF imejipanga kutoa semina kwa wanachuo mbalimbali ambayo wanatarajia kuingia katika soko la ajira hasa wanaoajiriwa na serikali ili kuweza kupata mafao bora pindi wakapofikia umri wa kustaafu.








Read More...

Wednesday, April 17, 2013

WAWILI WAJINYONGA MANISPAA YA MUSOMA





Mwanamke aliyejulikana kwa jina moja la Bhoke au mama Marwa  Mkazi wa Mtaa wa Ghandhi  Manispaa ya Musoma akiwa amejitundika chumbani kwake mtaa wa Ghandi Manispaa ya Musoma

 Polisi na wananchi wa Musoma wakimtoa nguo shingoni na kumuweka vizuri Marehemu Bhoke au mama Marwa  kwa ajili ya kumpeleka Katika Hospitali ya Mkoa wa Mara kwa ajili ya Taratibu zingine za kuhifadi mwili wake na mazishi.




Na Thomas Dominick,
Musoma
 
WANAWAKE wawili katika  Manispaa ya Musoma maeneo tofauti  wamejinyonga  huku mmoja akijinyonga kwa kutumia  mkanda wa suruali na mwingine akijinyonga kwa kutumia  mtandio.

Katika tukio la kwanza mwanamke  aitwaye Rudia kyango umri wa miaka 40 Mkazi wa kata ya Kigera  Manispaa ya Musoma  amekutwa amekufa baada ya kujinyonga kwa kutumia  mkanda wa suruali.

Kutokana na kujiua kwa mwanamke huyo ndugu na jamaa na jirani zake wamebaki na simanzi kubwa.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia April 13 mwaka huu ambapo marehemu alijinyonga kwa  kutumia mkanda wa suruali na kufariki dunia.

Wakazi wa eneo hilo walifika nyumbani kwa marehemu na kutoa taarifa  katika kituo kidogo cha Polisi Kigera kuuchukua mwili wa marehemu kwa  kwa ajili ya uchunguzi katika Hospitali ya Mkoa wa Mara.

Wakati huo huo Mwanamke mwingine aliyejulikana kwa jina moja la Bhoke au mama Marwa  Mkazi wa Mtaa wa Ghandhi  Manispaa ya Musoma mwenye umri kati ya miaka 27 hadi 30 amejiua kwa kujinyonga kwa kutumia mtandio akiwa chumbani kwake.

Tukio hilo limetokea asubuhi  leo (jana)  katika mtaa wa ghandi mjini Musoma baada ya watoto wake kwenda shuleni  baada ya majirani kuona mwenendo wake sio mzuri walitoa taarifa polisi.

Majirani hao waliiambia mwandishi wa Blog hii kuwa Mwanamke huyo huenda alichukua maamuzi hayo baada ya watoto wake kwenda shuleni na kubaki pekee yake nyumbani.

Umati wa watu wa Manispaa  ya Musoma ulijaa katika eneo la tukio  huku simanzi zikitawala kufuatia kifo hicho cha kujinyonga  ambapo  marehemu kabla ya kifo chake alikuwa anafanya kazi kwa mtu binafsi ya kuuza  vinywaji baridi.

Jeshi la polisi  lilifika katika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi  wa  kitabibu ili kubaini  kilichopelekea kifo cha marehemu huyo.

MWISHO

Read More...