*Wanachuo hao wataka umri wa kustaafu ushuke hadi miaka 40
*PSPF yajenga nyumba kwa ajili ya kuwakopesha wanachama wao
*Vijana wapendelewa zaidi na mfuko huo
Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma Sudi Hamza akiandika fomula ya kupata mafao kwa wanachuo wa chuo cha ualimu Bunda wanaotarajia kuanza mitihani yao mei 6 mwaka huu na kupata ajira ya Serikali
Wanachuo wa chuo cha Ualimu Bunda wakimsikiliza kwa makini Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma Sudi Hamza katika semina ya siku moja chuoni hapo.Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma Sudi Hamza akiwaelezea wanachuo wa chuo cha Bunda umuhimu wa kujiunga na mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma na mafao ambayo wanaweza kupata wakiwa wananchama wa mfuko huo.
Wanachuo wa Chuo cha Ualimu Bunda wakipata soda baada ya kumalizikia semina ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma PSPF iliyofanyika chuoni hapo ili kuwajengea uwezo wa kuufahamu vizuri mfuko huo..
Wanachuo wakisoma vipeperushi vya Mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa Umma (PSPF) katika semina ya siku moja iliyofanyika chuoni hapo.
Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa Umma (PSPF) Mkoa wa Mara Sudi Hamza akitoa formula kwa wanachuo wa Chuo cha Ualimu Bunda jinsi ya kupata mafao yako ya uzee baada ya kustaafu.
Wanachuo wa chuo cha Ualimu bunda wakimsikiliza Afisa Mfawidhi wa PSPF Sudi Hamza wakati wa semina ya siku moja kwa ajili ya kuwajengea uwezo na uelewa wa mfuko huo.
Na Thomas Dominick,
Bunda
MFUKO wa Pensheni kwa
Watumishi wa Umma (PSPF) umewajengea uwezo na ufahamu wa mfuko huo wa Pensheni wanachuo
wa Chuo cha Ualimu Bunda kilichopo wilaya ya Bunda Mkoani Mara wanaotarajia
kuajiriwa na Serikali mwaka huu.
Akitoa semina ya siku moja chuoni hapo Afisa Mfawidhi wa PSPF Mkoa wa huo, Sudi Hamza
aliwataka wanachuo hao wanaotarajia kuanza mitihani ya mwisho mei 6 mwaka huu kuwa
makini na mifuko hiyo pindi watakapoajiri na Serikali.
“Nimekuja chuoni hapa kwa
ajili ya kufanya semina na ninyi ili kuwapatia ufahamu wa na kuwaongezea uwezo
wa kuutambua vizuri mfuko wa PSPF na kujua faida ya kujiunga nao kwani ndio
unaotoa faida kubwa kwa wanachama wake,”alisema Hamza.
Baada ya Hamza kuwasilisha
mada juu ya mfuko huo wanachuo hao walipewa nafasi ya kuuliza maswali na
mapendekezo mbalimbali ambayo yangeweza kuwajenga zaidi.
Ambapo mwanchuo aliyejulikana
kwa jina la Kinguye Wambura aliiomba PSPF kwa kushirikiana na Serikali kujadili
kwa kina juu ya umri wa kustaafu kwa watumishi kutoka miaka 55 ya hiari na 60
ya lazima hadi kufikia 40 hadi 45.
“Hii hali ya kusubiria hadi
miaka 55 na 60 ni ni uonevu kwa watumishi kwani hadi kufikia umri huo mtumishi
anakuwa hana nguvu ya kufanya biashara na akili inakuwa imechoka haitamnufaisha
fedha hiyo kwani akili inakuwa imechoka hivyo Serikali ipunguze miaka hadi 40
na 45 ya lazima,” alisema Wambura.
Naye mwanachuo
aliyejitambulisha kwa jina la Agnes Ezekiel alimuuliza Afisa huyo kuwa kama
kuna uwezo wa kujiunga na mifuko zaidi ya mmoja kwa ajili ya kupata mafao mengi
pindi atakapostaafu.
Hamza alimjibu kuwa hiyo haiwezekani kujiunga na mfuko zaidi
ya mmoja labda ajiunge na Mfuko wa Hiari uliopo chini ya PSPF ambapo atalipwa
mafao yake baada ya kuwekeza ambapo fedha hiyo isipungue sh. 10,000/= kwa
mwezi.
Alisema kuwa pia PSPF inatoa
mafao ya Elimu ambapo kama mwanachama anataka kwenda kusoma yeye ama motto wake
unampatia fedha hizo kwa ajili ya kulipia ada, aliongeza kuwa PSPF inatoa mafao
ya ujasiriamali kwa mwanachama ambaye anataka kuanzisha biashara.
Pia alisema kuwa PSPF
inajenga nyumba sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuwakopesha wanachama wake waliotimiza
miaka mitano ili kuwakwamua kimaisha ambapo mwanachama atatakiwa kulipa ndani
ya miaka 25.
“Kutokana na kujua ugumu wa maisha
tumeamua kujikita katika kujenga nyumba bora za kisasa kwa ajili ya kuwakopesha
wanachama wetu ambazo watalipa ndani ya mika 25 na sharti kuu lazima atomize
miaka mitano kazini,”alisema.
Hamza aliwatoa wasiwasi
wanachuo kuwa serikali imeweka ofisi kila mkoa kwa ajili ya kupunguza usumbufu
kwa wanachama wao kusafiri kufuatilia mafao yao Makao Makuu Dar es Salaam na
kufuata ushauri na maelekezo mbalimbali.
Kwa sasa mtumishi akiwa na
shida hana haja ya kwenda Makao Makuu ya PSPF anachotakiwa ni kwenda makao
makuu ya Mkoa kwani kila mkoa kuna ofisi yetu kwa ajili ya ushauri na kama una
tatizo linamalizikia hapo tena bila usumbufu wowote,”alisema.
PSPF imejipanga kutoa semina
kwa wanachuo mbalimbali ambayo wanatarajia kuingia katika soko la ajira hasa wanaoajiriwa
na serikali ili kuweza kupata mafao bora pindi wakapofikia umri wa kustaafu.
0 comments:
Post a Comment