Wednesday, April 17, 2013

WAWILI WAJINYONGA MANISPAA YA MUSOMA





Mwanamke aliyejulikana kwa jina moja la Bhoke au mama Marwa  Mkazi wa Mtaa wa Ghandhi  Manispaa ya Musoma akiwa amejitundika chumbani kwake mtaa wa Ghandi Manispaa ya Musoma

 Polisi na wananchi wa Musoma wakimtoa nguo shingoni na kumuweka vizuri Marehemu Bhoke au mama Marwa  kwa ajili ya kumpeleka Katika Hospitali ya Mkoa wa Mara kwa ajili ya Taratibu zingine za kuhifadi mwili wake na mazishi.




Na Thomas Dominick,
Musoma
 
WANAWAKE wawili katika  Manispaa ya Musoma maeneo tofauti  wamejinyonga  huku mmoja akijinyonga kwa kutumia  mkanda wa suruali na mwingine akijinyonga kwa kutumia  mtandio.

Katika tukio la kwanza mwanamke  aitwaye Rudia kyango umri wa miaka 40 Mkazi wa kata ya Kigera  Manispaa ya Musoma  amekutwa amekufa baada ya kujinyonga kwa kutumia  mkanda wa suruali.

Kutokana na kujiua kwa mwanamke huyo ndugu na jamaa na jirani zake wamebaki na simanzi kubwa.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia April 13 mwaka huu ambapo marehemu alijinyonga kwa  kutumia mkanda wa suruali na kufariki dunia.

Wakazi wa eneo hilo walifika nyumbani kwa marehemu na kutoa taarifa  katika kituo kidogo cha Polisi Kigera kuuchukua mwili wa marehemu kwa  kwa ajili ya uchunguzi katika Hospitali ya Mkoa wa Mara.

Wakati huo huo Mwanamke mwingine aliyejulikana kwa jina moja la Bhoke au mama Marwa  Mkazi wa Mtaa wa Ghandhi  Manispaa ya Musoma mwenye umri kati ya miaka 27 hadi 30 amejiua kwa kujinyonga kwa kutumia mtandio akiwa chumbani kwake.

Tukio hilo limetokea asubuhi  leo (jana)  katika mtaa wa ghandi mjini Musoma baada ya watoto wake kwenda shuleni  baada ya majirani kuona mwenendo wake sio mzuri walitoa taarifa polisi.

Majirani hao waliiambia mwandishi wa Blog hii kuwa Mwanamke huyo huenda alichukua maamuzi hayo baada ya watoto wake kwenda shuleni na kubaki pekee yake nyumbani.

Umati wa watu wa Manispaa  ya Musoma ulijaa katika eneo la tukio  huku simanzi zikitawala kufuatia kifo hicho cha kujinyonga  ambapo  marehemu kabla ya kifo chake alikuwa anafanya kazi kwa mtu binafsi ya kuuza  vinywaji baridi.

Jeshi la polisi  lilifika katika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi  wa  kitabibu ili kubaini  kilichopelekea kifo cha marehemu huyo.

MWISHO

0 comments:

Post a Comment