Monday, October 21, 2013

UCHOMAJI MOTO MISITU WILAYA YA NANYUMBU SASA WAVALIWA NJUGA TAASISI ZAANZA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI WA WILAYA HIYO



Na Thomas Dominick,

Nanyumbu



BAADA ya Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Festo Kiswaga kutangaza kuwa uchomaji moto misitu ni janga la wilaya hiyo taasisi mbalimbali zimeanza kutoa mafunzo juu ya athari za uchomaji moto misitu kwa kushirikiana na Halmashauri hiyo.



Akizungumza na mwandishi wa habari ofisini kwake jana, Afisa Misitu wa wilaya hiyo Fokas Mlelwa alisema kuwa halmashauri hiyo kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu ambayo makao makuu yake yapo Wilayani Masasi wameweza kutoa elimu katika vijiji vinne vinavyozunguka Misitu ya Taifa za Ndechela na Mbangara.



Alisema kuwa vijiji vilivyonufaika na mafunzo hayo ni kijiji cha Mburusa na Chimika vilivyo katika hifadhi ya Ndechela na kijiji cha Marumba na Mbangara Mbuyuni vilivyo katika hifadhi ya Mbangara.



“Mafunzo yetu yameshirikisha rika mbili za wazee na vijana ambapo kila kijiji kilifanya mafunzo kwa siku moja ambapo tulianza na wazee 10 kisha vijana 10 ambapo mada kuu ilikuwa moto na jamii,”alisema Mlelwa.



Alisema kuwa kundi la wazee walifundishwa na kulenga kupunguza matukio ya moto na wazee hao waliweka mikakati mbalimbali pamoja na kuunda kamati za kusimamia na kupunguza matukio ya moto katika maeneo yao.



Pia alisema kuwa vijana nao walifundishwa masomo kama ya wazee lakini ya ziada walifundishwa mbinu mbalimbali za kukabiliana na moto unapotokea na kuuzima, pia mbinu ya namna ya kuuzima moto, vifaa, namna ya kumuokoa mtu aliyezingirwa na moto na mbinu ya kujiokoa mwenyewe na moto.



Alisema kuwa uchomaji wa moto misitu unasababisha harasa kubwa kwa jamii ambapo huatarisha uhai wa watu, mali na mzaingira yao, vyanzo vya maji hubakia wazi na kusababisha kukauka, uoto wa asili unapotea na uhai wa viumbe hai nao unapotea.



Alipoulizwa kuwa mafunzo hayo yatasaidia kumaliza tatizo la uchomaji moto misitu mwakani na kunahatua gani watavifikia vijiji vingine Mlelwa alisema kuwa mafunzo hayo hayataweza kutokomeza kabisa tatizo la uchomaji moto lakini yatasaidia kupunguza matukio ya moto ambayo yameshamiri wilayani humo.



“Mpango wetu ni kuvifikia vijiji vyote vilivyopo wilaya yetu kwani tatizo hili linavikabili vijiji vingi sana katika wilaya yetu lakini tatizo la kifedha ndio kikwazo kikubwa kwetu lakini tukipata fedha tutafaya mafunzo hatua kwa hatua ili tuvifikie vijiji vyote na kutokomeza kabisa janga hili,”alisema Mlekwa.



     














Read More...

NDONDOCHA HAI APATIKANA KIJIJI CHA LUKULEDI WILAYA YA MASASI MKOA WA MTWARA TAFARANI KUBWA YAZUKA POLISI WAKANA KUHUSIANA NA TUKIO HILO



Na Thomas Dominick,
Masasi

Hali ya wasiwasi imeikumba kijiji cha Lukuledi Wilaya ya Masasi Mkoa wa Mtwara baada ya kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Said Nitole (18) ambaye alipotea katika mazingira ya utatanishi takribani miaka mitatu na kudaiwa kuchukuliwa ndondocha amepatikana akiwa amefungwa dawa kifuani, kiunoni na sehemu za siri.

Wakingumza na mwandishi wa habari kijijini hapo mashuhuda wa tukio hilo ambaye ni mwanamgambo aliyejitaja kwa jina la Bonifance Lukas na mwalimu wa Shule ya msingi Lukuledi Rita Mbunda walisema kuwa tukio hilo lilitokea Octoba 18 mwaka huu baada ya kijana huyo kufika kwa mganga wa kienyeji aliyejulikana kwa jina la Mama Kongo na kulia kama paka kisha kutoweka.

Walidai kuwa siku ya pili octoba 19 saa moja usiku alifika tena kisha kuongea kwa lugha ya ishara ambapo mganga huyo alifanya dawa zake na kumdhibiti asitoweke kisha alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa serikali ya kijiji Said Makota na kituo kidogo cha polisi.

“Baada ya kutoa taarifa watu wengi walikusanyika na mimi kama mwanamgambo wa kijiji nilimchukua sambamba na viongozi pamoja na askari polisi hadi kituoni kwa mahojianao zaidi,”alisema Lucas.

Alidai kuwa baada ya mahojiano kijana huyo alisema kuwa alikuwa kwa mmoja wa wafanyabiashara yeye na wenzake wengine wengi wakimfanyia kazi mbalimbali ikiwemo kazi za kilimo na kuokota korosho ambapo alisema kuwa kwa siku yeye peke yake alikuwa anaokota debe tano,

Wananchi waliofika eneo la kituoni walipandisha jazba na kuomba uongozi wa kijiji pamoja na askari wawapeleke walipo ndondocha wengine ili waweze kuwatoa kisha kumfanyia kitu kibaya mhusika wa matukio hayo.

Mkuu wa kituo hicho baada ya kuona hali ni tete aliomba msaada kutoka kituo kikuu cha Polisi wilayani Masasi kwa ajili ya kuweka ulinzi pamoja na kumchukua kijana huyo kwa mahojiano zaidi.

Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho Said Makota naye alikiri kuwa tukio hilo la kushangaza lilitokea kijiji hapo ambapo mzazi wa kijana huyo aliyemtaja kwa jina la Rashid Nitole aliwahi kutoa taarifa za kupotea kwa kijana wake katika mazingira ya utatanishi kisha kupatiwa kibali cha kumtafuta sehemu mbalimbali.

“Lakini baada ya kupatikana kwa kijana huyo mwishoni mwa wiki tulimtafuta mzazi wa mtoto huyo na baada ya kufika alimtambua mtoto wake na mtoto alimtambua baba yake kisha walikumbatiana,”alisema Makota.

Alisema kuwa madai ya kuwa alikuwa kwa mmoja wa wafanyabiashara wa kijiji hicho mwenyekiti huyo alipinga na kusema kuwa ndondocha huyo alitokea kwa mganga wa kienyeji na sio kwa mfanyabiashara.

Taarifa kutoka kituo kikuu cha Polisi Wilaya ya masasi zilisema kuwa wao walienda kutoa ulinzi lakini hawawezi kulisemea suala hilo kwani polisi halihusiani na masuala ya kishirikina.



































Read More...

Friday, September 20, 2013

MWENGE UMEFUNGUA, UMEZINDUA NA KUKAGUA, YAWEKA JIWE LA MSINGI MIRADI 11 YENYE THAMANI YA TSHS MILIONI 672.922 WIALAYA YA NANYUMBU MKOA WA MTWARA






 MKUU WA WILAYA YA NANYUMBU FESTO KISWAGA AKIMSIKILIZA MMOJA WA KIONGOZI WA WILAYA HIYO KATIKA SHEREHE ZA UPOKEAJI WA MWENGE KATIKA KIJIJI CHA ULANGA WILAYANI HUMO UKITOKEA WILAYA YA MASASI.


 WANANCHI WA WILAYA YA NANYUMBU MKOA WA MTWARA WAKIWA KATIKA SHANGWE KUBWA KWA AJILI YA KUUPOKEA MWENGE WA UHURU UNAOTOKEA WILAYA YA MASASI.

 WANANCHI WA WA WILAYA YA NANYUMBU WAKIWA WAMEFURIKA KATIKA KIJIJI CHA NANYUMBU KUUPOKEA MWENGE WA UHURU ULIOTOKEA WILAYA YA MASASI.


 MKUU WA WILAYA YA NANYUMBU FESTO KISWAGA AKIWA KATIKA VIWANJA VYA MAKABIDHIANO YA MWENGE WA UHURU KATIKA KIJIJI CHA ULANGA WILAYANI HUMO.
 MWENGE WA UHURU UKIWASIRI KATIKA KIJIJI CHA ULANGA MPAKANI MWA MASASI NA NANYUMBU KWA AJILI YA KUANZA MBIO ZAKE WILAYA YA NANYUMBU.

 MKUU WA WILAYA YA NANYUMBU FESTO KISWAGA AKISALIMIA NA MMOJA WA WAKIMBIZA MWENGE BAADA YA KUWAPOKEA WAKITOKEA WILAYA YA MASASI
  MKUU WA WILAYA YA NANYUMBU FESTO KISWAGA AKIKUMBATIANA NA MMOJA WA WAKIMBIZA MWENGE WA KITAIFA KATIKA KIJIJI CHA ULANGA BAADA YA KUKABIDHIWA KUTOKEA WILAYA YA MASASI
  MKUU WA WILAYA YA NANYUMBU FESTO KISWAGA AKIWA NA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE JUMA ALI SIMAI WAKIMSIKILIZA MKUU WA WILAYA YA MASASI
 MKUU WA WILAYA YA MASASI FATUMA AKIWA AMEUSHIKA MWENGE WA UHURU TAYARI KUMKABIDHI MKUU WA WILAYA YA NANYUMBU FESTO KISWAGA.
 MKUU WA WILAYA YA MASASI FATUMA AKIZUNGUMZA JAMBO FULANI KABLA YA KUMKABIDHI MWENGE WA UHURU MKUU WA WILAYA YA NANYUMBU FESTO KISWAGA.
 MKUU WA WILAYA YA NANYUMBU FESTO KISWAGA AKIPOKEA MWENGE WA UHURU KUTOKA KWA MKUU WA WILAYA YA MASASI FATUMA
 MKUU WA WILAYA YA NANYUMBU FESTO KISWAGA AKISEMA JAMBO BAADA YA KUPOKEA MWENGE WA UHURU TOKA KWA MKUU WA WILAYA YA MASASI FARIDA MGOMI ALIYEINAMIA CHINI

 MWENGE WA UHURU UKIWA UMEANZA MBIO ZAKE WILAYA YA NANYUMBU BAADA YA KUTOKA WILAYA YA MASASI
 MKUU WA WILAYA YA NANYUMBU FESTO KISWAGA AKIMSIKILIZA MMOJA WA WAKIMBIZA MWENGE KITAIFA KATIKA UFUNGUZI WA BARABARA YA NANDETE CHIVIRIKITI.
 KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE JUMA ALI SIMAI AKIFUNGUA GHALA LA KUHIFADHIA MAZO KATIKA KIJIJI CHA MCHANGANI A WILAYA YA NANYUMBU MKOA WA MTWARA.

 KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE JUMA ALI SIMAI AKIKRIKI KWENYE KOMPUTA WAKATI AKIFUNGUA KITUO CHA WALIMU KATA YA MIKANGAULA.

 MKUU WA WILAYA YA NANYUMBU FESTO KISWAGA AKIPANDA MTI KWENYE CHANZO CHA MAJI KATIKA KIJIJI CHA NANGOMBA KWENYE BUSTANI YA VIJANA YA MBOGAMBOGA
 KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE JUMA ALI SIMAI AKIFUNGUA MAJI WAKATI AKIZINDUA MRADI WA MAJI SAFI NA SALAMA KATIKA KIJIJI CHA NDWIKA WILAYANI NANYUMBU

 WANANCHI WA WILAYA YA TUNDURU MKOA WA RUVUMA WAKICHEZA KATIKA MAKABIDHIANO YA MWENGE WA UHURU AMBAO ULIKUWA UNATOKA MKOA WA MTWARA NA KUINGIA MKOA WA RUVUMA KATIKA KIJIJI CHA SAUTI MOJA KILICHOPO MPAKANI MWA WILAYA YA NANYUMBU NA TUNDURU
 MKUU WA WILAYA YA NANYUMBU FESTO KISWAGA AKIMKABIDHI MKUU WA MKOA WA MTWARA KANALI JOSEPH SIMBAKALI KABLA YA KUUKABIBHI KWA MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAIDI MWAMBUNGU KWA AJILI YA KUANZA MBIO ZAKE KATIKA WILAYA YA TUNDURU MKOA WA RUVUMA.
MKUU WA MKOA WA MTWARA JOSEPH SIMBAKALI AKIMKABIDHI MWENGE WA UHURU MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU.  


Na Thomas Dominick,
Nanyumbu

MIRADI 11 yenye thamani ya Milioni 672.922 imefungua na kuweka jiwe la msingi, Kukagua na kuzindua na Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Nanyumbu, Mkoa wa Mtwara.

Akisoma risala ya utii ya wananchi wa wilaya hiyo kwa Rais wa Jakaya Kikwete, mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge Juma Ali Simai Mkuu wa wilaya hiyo Festo Kiswaga alisema kuwa miradi hiyo inatoka katika sekta ya miundombinu, elimu ya msingi na sekondari, kilimo, maji, Nishati, ujasiriamali na utawala bora.

“Miradi hiyo iliyotekelezwa ilipata fedha kutoka katika vyanzo mbalimbali ambapo nguvu za wananchi zilikuwa Tshs Milioni 268.238, Serikali kuu tshs. Milioni 325.026, Halmashauri ya wilaya tshs milioni 62.113 na wahisani tshs. Milioni 17.544,”alisema.

Alisema kuwa katika mgawanyo sawa wa rasilimali wilya hiyo inajitahidi kuzingatia uwiano katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii na za kiuchumi katika kata 14 kupitia miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye ngazi hiyo.

“Aidha tumekuwa makini kuhakikisha kwamba watumishi wanaopangiwa wilayani kwetu wanagawanywa kwa uwiano unaozingatia mahitaji kwenye maeneo husika kama vile walimu wa shule za msingi na sekondari, wataalam wa afya, watendaji vijiji na kata,”alisema Kiswaga.

Alisema kuwa pamoja na mafanikioya wilaya hiyo pia kuna changamoto zinazowakabili ambazo zinahitaji msukumo na ufunbuzi wa kitaifa, ambapo moja ya changamoto hizo ni tatizo la upatikanaji wa maji safi na salam.

“Kwa sasa asilimia 28.7 tu ya wananchi wanapata maji safi na salama pia tuna upungufu wa watumishi wenye taaluma mbalimbali aidha wilaya ina uhaba wa vyombo vya usafiri hususani magari kwa ajili ya matumizi ya ofisi kwenye idara mbalimbali,”alisema.

Mwenge huo ulipokelewa katika Kijiji cha Ulanga kukimbizwa kilometa 124 na kukabidhiwa katika kijiji cha shauri moja mpakani mwa wilaya hiyo na mkoa wa ruvuma.

Miradi iliyopitiwa na mwenge huo ni ujenzi wa barabara kutoka Nandete hadi Chivirikiti yenye urefu wa Kilometa 7, madarasa mawili katika shule ya sekondari maratani, ghala la kuhifadhia mazao kijiji cha mchangani na kituo cha uendelezaji walimu (TRC).

Mingine ni upandaji miti kwenye chanzo cha maji nangomba, kilimo cha bustani za mbogamboga kinachoendeshwa na vijana wa nangomba, maji ya bomba ndwika, kituo cha mafuta cha Kinjikitile, banda la mama wajasiriamali, Afya, ukimwi, polisi na dawa za kulevya na banda la TAKUKURU yote ya mjini mangaka.


MWISHO

Read More...

Saturday, September 14, 2013

TASAF YAMWAGA BILION 1.7 KATIKA MIRADI MBALIMBALI WILAYA YA NANYUMBU MKOA WA MTWARA.






 Vijana Kikundi cha sanaa cha mjini mwema wakionesha umahiri wao mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais mahusiano na Uratibu Stevin Wasira aliyefika katika kijiji hicho kwa ajili ya kukagua mradi wa miti kwa ajili ya kulinda vyanzo vya maji
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais mahusiano na Uratibu Stevin Wasira akisalimiana na viongozi wa kijiji cha Michiga ndani ya wilaya ya Nanyumbu.
 Wananchi wa Msinyasi wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais mahusiano na Uratibu Stevin Wasira(hayupo pichani) baada ya kukagua mradi wa barabara iliyounganisha kati ya kijiji cha magomeni na msinyasi yenye urefu wa KM 9.8
 Moja ya ufadhili wa TASAF wa umeme wa jua katika shule ya sekondari ya Sengenya
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Stevin Wasira akisikiliza risala ya kikundi cha wajane na wagane wa kikundi cha ufugaji kuku katika kijiji cha ngalinje.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais mahusiano na Uratibu Stevin Wasiraakimsikiliza mjane Hadija Mrope kabla ya kukagua mradi wa ufugaji wa kuku uliofadhiliwa na TASAF katika kijiji cha Ngalinje Wilaya ya Nanyumbu Mkoa wa Mtwara.
 Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya nanyumbu wakimsilikiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais mahusiano na Uratibu Stevin Wasira kwenye ukumbi wa mikutano wa mkuu wa wilaya.
 Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mkoa wa Mtwara Festo Kiswaga akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais mahusiano na Uratibu Stevin Wasira alipowasili wilayani humo kwa ajili ya ziara ya siku moja kukagua na kujionea shughuli za maendeleo ya wananchi kwa ufadhili wa TASAF.



Na Thomas Dominick,
Nanyumbu

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)  awamu ya pili umetoa jumla ya Tshs Bilioni  1.7 kwa ajili ya kufadhili miradi 85 katika vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Nanyumbu, Mkoa wa Mtwara.

Akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya wilaya hiyo kwa Waziri wa Nchi  ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Stevin Wasira aliyekuwa katika ziara ya kukagua miradi iliyofadhiliwa na TASAF Mkuu wa wilaya Festo Kiswaga alisema kuwa TASAF imesaidia kuinua maisha ya wananchi ya wilaya hiyo katika nyanja mbalimbali.

Kiswaga alisema kuwa jumla ya miradi 75 imekamilika na miradi ambayo ipo katika hatua ya utekelezaji ni miradi 10 iliyoanza Julai mwaka huu na pia kuna miradi 14 inayosubiri fedha kutoka TASAF.

“Miradi iliyokuwa katika hatua ya utekelezaji ni miradi sita ya ujenzi wa barabara, miradi mitatu ya uhifadhi wa mazingira na mradi mmoja wa hifadhi msitu shirikishi,”alisema Kiswaga.

Pia alisema kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa, nyumbza za walimu, zahanati na mabweni kwa shule za sekondari.

“Hivyo watoto wanasoma katika mazingira magumu na pia walimu kufundisha katika mazingira magumu na duni hii inachangia kushuka kwa elimu,” alisema.

Mkuu huyo wa wilaya alitumia fursa hiyo kuiomba TASAF ione uwezekano wa kuiwezesha Halmashauri hiyo kutatua tatizo hilo kwani serikali inajitahidi kuwashirikisha wananchi katika mipango mbalimbali ya maendeleo.

Naye Waziri Wasira aliwaomba wananchi kutumia fursa zinazotolewa na serikali ili kuweza kujiletea maendeleo yao wenyewe na kujikwamua kutoka katika umasikini uliokithiri katika jamii.

“Mipango ya TASAF ni endelevu ili kuwainua wananchi wetu kutoka katika umasikini na kuishi maisha  mazuri pia tunawashauri wataalamu wetu kuwa karibu na wananchi kuwapatia mafunzo bora ya kilimo, ufugaji na uzalishaji mali,”alisema Wasira  

Wasira aliwaomba viongozi wa TASAF alioambatana katika ziara hiyo wanatakiwa kujifunza na kuona matatizo yanayowakabili wananchi na kufikiria zaidi familia maskini.

Miradi aliyotembelea ni pamoja na kikundi cha ufugaji kuku cha wajane na wagane kilichopo kijiji cha Ngalinje, ujenzi wa barabara kuunganisha kijiji cha magomeni na msinyasi na barabara yenye urefu wa Km 4 inayounganisha kitongoji cha Mikangaula na kijiji cha Nakopi.

Miradi mingine ni ujenzi wa masijala ya kutoa hati miliki katika kijiji cha michiga na  mradi wa kupanda miti kwenye vyanzo vya maji katika kijiji cha Nangomba ambapo kwa sasa kuna vitalu takribani 20 na wanatarajia kupanda miti hiyo mwezi Desemba mwaka huu.


Read More...

Thursday, August 22, 2013

WANANCHI WA KATA YA KIAGATA WILAYA YA BUTIAMA MKOA WA MARA WAOMBA JIMBO LIGAWANYWE, MILONI 420 ZA MADENI ZAWAGAWA MADIWANI

MKUU WA MKOA WA MARA JOHN TUPPA AKIMKABIDHI KAIMU MKURUGENZI RICHARD MIHAYO HATI YA KUDHIBITISHWA KWA HALMASHAURI MPYA YA BUTIAMA ILIYOZALIWA KUTOAKA HALMASHAURI YA MUSOMA.
MKURUGENZI MPYA WA HALMASHAURI YA BUTIAMA RICHARD MIHAYO AKIWA PAMOJA NA HATI YA UANZISHWAJI KWA HALMASHAURI HIYO.


 Na Thomas Dominick

 Butiama



 WANANCHI wa Tarafa ya Kiagata Wilaya ya Butiama, Mkoa wa Mara wameiomba Serikali kuipatia Kata hiyo  jimbo linalojitegemea kutokana na  jimbo la Musoma Vijijini linalotawaliwa na Mbunge Nimrod Mkono kuwa kubwa na kushindwa kufikisha huduma muhimu kwa wananchi.



 Akitoa hoja hiyo katika kikao maalum cha uvuvunjaji wa Halmashauri hiyo na kuzaa Halmashauri mpya ya Butiama, Diwani wa Kata ya Buswahili, Tarafa ya Kiagata Kawaki Marwa  alisema kuwa kutokana na ukubwa wa eneo hilo imekuwa vigumu kuwafikishia huduma muhimu kwa wakazi wa maeneo hayo kufika.



 “Mheshimiwa Mwenyekiti eneo la Kiagata ni kubwa sana, tunaomba sisi kama wananchi wa maeneo hayo Serikali ilikate jimbo hilo na tuwe na majimbo mawili ili kuweza kuwafikishia huduma wananchi kirahisi kuliko ilivyokuwa sasa,”alisema Marwa



 Alisema kuwa Tarafa hiyo ina kata nne na wakazi 35,274 kwa takwimu za sensa iliyofanyika mwaka 2012, nchi mzima kitu ambacho kimesababisha huduma zinazotolewa na mbunge huyo kuwa zinawanufaisha wananchi wa upande mmoja na upande mwingine kuteseka.



 Naye Mkuu wa Mkoa huo John Tuppa wakati akitoa hotuba kabla

 ajakadhidhi hati ya kuashiria uanzishwaji wa Halmashauri hiyo mpya ya Butiama kwa Kaimu Mkurugenzi Richard Mihayo alisema kuwa Halmashauri ya Musoma ina eneo kubwa hivyo inahitaji kupata majimbo mengine mawili.



 “Changamoto zilizokuwa zinaikabili Halmashauri hii ni ukubwa wa eneo na hapa tumeanza tu kugawa katika Halmashauri mbili lakini inatakiwa iwe na majimbo aidha matatu ya uchaguzi ili kuweza kuwaqfikishia huduma wananchi wa maeneo hao,” alisema Tuppa.



 Alisema kuwa pamoja na hilo viongozi wa Halmashauri hizo waache utendaji kazi wa mazoea ili waweze kuwatendea haki wananchi wao ikiwa pamoja na kuwatatulia kero mbalimbali zinazowakabili.



 Ugawaji wa Halmashauri hizo ilifanyika ikiwa ni pamoja na kugawana raslimali na madeni yaliyokuwepo katika Halmashauri hiyo hatua hiyo ambayo ilikwisha kwa amani na utulivu huku kila mjumbe akiridhia ugawaji huo.



 Hivi karibuni katika mchakato kama huo wa kugawa Halmashauri ya Tarime na Halmashauri ya Mji wa Tarime vurugu zilitokea kutokana na madiwani watatu wa viti maalumu wa CCM na Chadema kukataliwa kuingiwa Mjini kwa madai hawakai maeneo ya mjini na kusababisha kutoelewana na madiwani kurushia maneno na kuvunjiaka bila muafa.



 MWISHO











 Na Thomas Dominick

 Butiama.



 HALMASHARI ya Wilaya ya Musoma Mkoa wa Mara imejikuta katika wakati mgumu pale baada ya madiwani kuitaka halmashauri kutoa ufafanuzi wa kina juu ya malimbikizo ya madeni kubwa la Milioni 402 ambazo zimeweza kusababisha kuzorota kwa  suala zima la Maendeleo kwa wananchi.



 Wakichangia hoja mbalimbali hii leo katika  kikao maalum kilichokuwa na lengo la kujadili mgawanyiko wa rasirimali kati ya halmashauri ya wilayaya  Musoma pamoja na Butiama, Diwani wa kata ya Nyambono Grayson Mfungo amesema kuwa  malimbikizo ya milioni 402 ni mzigo mkubwa kwa Halmashauri kitendo ambacho kinaweza kukwamisha baadhi ya shuguli za kimaendeleo.



 Kambi ya upinzani walitaka kujua halmashauri ilikuwa wapi mpaka

 inafikia hatua ya malimbikizo kwa watendaji  wanaokaimu idara mbali mbali na kudai kuwa watakubaliana  na mgawanyiko wa raslimali endapo tu halmashauri itatoa majibu ya kuridhisha kuhusiana na suala hili.



 Akijibu hoja hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Musoma Fidelica Myovela, alikiri kuwa  halmashauri inakabiliwa na deni kubwa na sehemu kubwa ya deni hilo nikutokana na posho za kukaimu nafasi ya Ukuu wa Idara  ambapo zilistahili kulipwa kwa wakuu mbalimbali wa idara.



 Naye Mkuu wa Mkoa wa huo,  John Tuppa  alikiri kupokea taarifa za malimbikizo ya madeni na  amehaidi kulipeleka suala hilo katika

 serikari kuu sambamba na uwasilishwaji wa wakuu mbali mbali wa idara ili kuweza kuondokana na tatizo la ukaimu ambapo limekuwa

 likisababisha mzigo mkubwa Kwa halmashauri.



 Aidha alizitaka halmashauri  kuhakikisha kuwa zinaboresha  mapato yake ya ndani na kuziba mianya yote inayopita fedha hizo katika mifuko ya watu binafsi ili  kuepuka ongezeko la msaada wa kifedha kutoka serikali kuu.



 “Viongozi wanashindwa kusimamia sheria za ukusanyaji mapato na hicho ndicho chanzo cha upotevu wa mapato ya ndani utakuta viongozi wana vitabu bandia vya risti za kukusanyia fedha za serikali, viongozi kama hawa hawatufai,”alisema Tuppa.



 Halmashauri ya wilaya ya Musoma imeweza kujitenga rasmi na kuzaa wilaya mbili  Butiama pamoja na Musoma Vijijini inayopigiwa debe iitwe kwa jina Nyanja lengo kuu likiwa kurahisisha huduma kwa wananchi.





 MWISHO


Read More...

Saturday, August 17, 2013

SERIKALI YATANGAZA NEEMA KWA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI WA BUHEMBA WILAYA YA BUTIAMA MKOA WA MARA






 Baadhi ya viongozi waliohudhuria kikao cha kutangaziwa neema kwa wachimbaji wadogo wa madini wa Buhemba Wilaya ya Butiama Mkoa wa Mara katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya Angeline Mabula.
Mkuu wa Wilaya ya Butiama Angeline Mabula akizungumza na viongozi na waandishi wa Habari hawapo pichani juu ya serikali kutenga maeneo kwa wachimbaji wadogo wa madini wa Buhemba.

Na Thomas Dominick,
Butiama.

SERIKALI imeshatimiza ndoto za wachimbaji wadogo baada ya kutangaza kukamilisha kazi ya upimaji wa viwanja 35 venye ukubwa wa hekta 9.64 katika eneo la Rwabasi na Mirwa katika machimbo ya Buhema Mkoani Mara.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari wilayani humo, Mkuu wa wilaya Angeline Mabula alisema kuwa utengaji wa maeneo hayo ni baada ya hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo kwenye bunge la bajeti 2013/14 kuwa wachimbaji hao wanatengewa maeneo rasmi ya uchimbaji.

“Kutokana na ari kubwa ya watafutaji wakubwa wa madini kuchukua leseni katika wilaya ya Butiama kumekuweko na uhaba wa maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo, Hali hii ilizua malalamiko kutoka kwa wachimbaji hao ambao waliomba kutengewa maeneo rasmi ya uchimbaji katika eneo la Buhemba,”alisema Mabula.

Alisema kuwa kabla ya upimaji huo eneo hilo lilifanyiwa uchunguzi wa Kijiolojia, Kijiofizikia na Kijiokemia na wataalamu kutoka wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) kubaini kuwa eneo hilo lina miamba yenye dhahabu,”alisema.

Alisema kuwa zoezi hilo la upimaji lilikuwa shirikishi likihusisha wachimbaji na viongozi wa kata ya Buhemba na Mirwa ambapo kukamilika kwa zoezi hilo alitoa wito kwa wananchi wa Kata za Buhemba na Mirwa kutumia fursa hiyo vizuri kutuma maombi ya leseni kwa afisa madini mkazi wa Musoma kupitia vikundi vyao ushirika.

Pia aliwaagiza maafisa madini kuhakikisha kuwa leseni zinatayarishwa mapema kwa wale wote watakaoomba na wahusika wanaonyeshwa maeneo ya leseni zao kwa wakati, Pia alitoa wito kwa wachimbaji wadogo kujiepusha kabisa vitendo vya uvamizi wa maeneo yanayomilikiwa na watu wengine au mwekezaji, hususani eneo la STAMICO na mwekezaji Manjaro Resources ya nchini Australia.

Mabula aliwaomba wananchi wawe wavumilivu na watii wa sheria bila shurti hasa pale wanapokuwa na malalamiko kwa utatuzi wa kero zao unazingatiwa kwa kufuata sheria za nchi, ambapo pia aliahidi kuwa ofisi yake kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini kuendelea kuwatafutia wananchi maeneo zaidi ya uchimbaji.

Naye Kaminishi Msaidizi Madini Kanda ya Ziwa Salim Said Salim alisema kuwa ofisi yake itahakikisha wachimbaji wadogo wanapata leseni za madini ndani ya wiki moja bila kuwa na usumbufu wowote.

MWISHO
Read More...