Watendaji wa wilaya ya butiama wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Mpya ya Butiama Angelina Mabula wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya Serikali ya awamu ya nne ya Rais JK Kikwete, kuanzia mwaka 2005 hadi 2012.
Na Thomas Dominick,
Butiama
MFUKO wa wajasiliamali
unaofadhiliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Rais Jakaya Kikwete na
asasi mbalimbali za kibenki zimeweza kuwakwamua kiuchumi wakazi wa wilaya mpya
ya Butiama ambapo jumla ya bilioni 7.370 zilikopeshwa kwa wananchi.
Mafanikio hayo ya Serikili ya
awamu ya Nne inayoongozwa na Rais Kikwete kutoka mwaka 2005 hadi 2012
yalitangazwa na Mkuu wa wilaya hiyo ofisini kwake, Angelina Mabula wakati
akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Mabula alisema kuwa katika mfuko
wa wajasiriamali Vikundi 4 vya wajasiliamali vilipewa mikopo yenye thamani ya shilingi
milioni 180, Mfuko wa Jamii (TASAF) nao
ulitoa shilingi milioni 250 na kukuopeshwa vikundi 32 , Mfuko wa DASIP ulitoa
shilingi milioni 400 kwa vikundi 445 vya shamba darasa na benki ya NMB ilitoa
shilingi Bilioni 6.64 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamiina uchumi kwa
wajasiriamali.
“Mfuko wa wajasiriamali wa Rais
Kikwete ulitoa fedha kwa vikundi vinne ambavyo ni Mwangaza Saccos ya Buhemba
shilingi milioni 80, Imani Bwai (Kiriba) shilingi milioni 31, Mwamucha SACCOS
(Mugango) milioni 30 na Ujamaa (Kukirango) milioni 29,”alisema Mabula.
Alisema kuwa TASAF ilitoa fedha
kwa vikundi 32 kama ifuatavyo, vikundi vinne ya useremara viliwezeshwa
uanzishaji wa karakana na vifaa vyenye thamani ya milioni 38.335, vikundi vya
ushonaji na ufumaji viliwezeshwa vyereheni 26 vyenye thamani ya milioni 13.954,
vikundi viwili vya akina mama vya usagaji na imewezeshwa mashine mbili za
kusaga na kukoboa zenye thamani ya milioni 21.922.
“Vikundi vingine ni kikundi cha
walemavu cha ufundi baiskeli kilipata milioni 5.894 na kuanzisha karakana na
vifaa vya ufundi baiskeli, Kikundi kimoja cha wazee cha ufugaji ng’ombe 17
kilipatiwa jumla ya milioni. 9.090 zikiwa gharama za ng’ombe 5, ujenzi wa
banda, chakula cha nyongeza na tiba Vikundi vya ufugaji kuku 17 vilipatiwa
jumla ya milioni 112.078 na Vikundi vya ufugaji mbuzi wa maziwa 3 vilipatiwa
jumla ya milioni 20.261,”alifafanua.
Alisema pamoja na mifuko hiyo
halmashauri hiyo ipo katika vipaumbele mbalimbali katika kuwakwamua wananchi
wake kiuchumi ikiwa pamoja na Kujenga masoko mawili ya kisasa na stendi mbili
za mabasi katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma na Butiama.
“Kujenga miradi mikubwa ya
umwagiliaji yenye kuongeza fursa za ajira kwa vijana tayari maeneo ya uwekezaji
huo yameanishwa na Kukaribisha wawekezaji ili wajenge viwanda,”alisema.
Alisema kuwa zoezi la upimaji
liko katika hatua nzuri ili kuweka mji katika utaratibu wa mipango mji. Mara
taratibu zote zitakapokamilika matangazo yatatolewa kwenye vyo vya habari ili
kila mhitaji apate kiwanja bila usumufu.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment