Thursday, August 22, 2013

WANANCHI WA KATA YA KIAGATA WILAYA YA BUTIAMA MKOA WA MARA WAOMBA JIMBO LIGAWANYWE, MILONI 420 ZA MADENI ZAWAGAWA MADIWANI

MKUU WA MKOA WA MARA JOHN TUPPA AKIMKABIDHI KAIMU MKURUGENZI RICHARD MIHAYO HATI YA KUDHIBITISHWA KWA HALMASHAURI MPYA YA BUTIAMA ILIYOZALIWA KUTOAKA HALMASHAURI YA MUSOMA.
MKURUGENZI MPYA WA HALMASHAURI YA BUTIAMA RICHARD MIHAYO AKIWA PAMOJA NA HATI YA UANZISHWAJI KWA HALMASHAURI HIYO.


 Na Thomas Dominick

 Butiama



 WANANCHI wa Tarafa ya Kiagata Wilaya ya Butiama, Mkoa wa Mara wameiomba Serikali kuipatia Kata hiyo  jimbo linalojitegemea kutokana na  jimbo la Musoma Vijijini linalotawaliwa na Mbunge Nimrod Mkono kuwa kubwa na kushindwa kufikisha huduma muhimu kwa wananchi.



 Akitoa hoja hiyo katika kikao maalum cha uvuvunjaji wa Halmashauri hiyo na kuzaa Halmashauri mpya ya Butiama, Diwani wa Kata ya Buswahili, Tarafa ya Kiagata Kawaki Marwa  alisema kuwa kutokana na ukubwa wa eneo hilo imekuwa vigumu kuwafikishia huduma muhimu kwa wakazi wa maeneo hayo kufika.



 “Mheshimiwa Mwenyekiti eneo la Kiagata ni kubwa sana, tunaomba sisi kama wananchi wa maeneo hayo Serikali ilikate jimbo hilo na tuwe na majimbo mawili ili kuweza kuwafikishia huduma wananchi kirahisi kuliko ilivyokuwa sasa,”alisema Marwa



 Alisema kuwa Tarafa hiyo ina kata nne na wakazi 35,274 kwa takwimu za sensa iliyofanyika mwaka 2012, nchi mzima kitu ambacho kimesababisha huduma zinazotolewa na mbunge huyo kuwa zinawanufaisha wananchi wa upande mmoja na upande mwingine kuteseka.



 Naye Mkuu wa Mkoa huo John Tuppa wakati akitoa hotuba kabla

 ajakadhidhi hati ya kuashiria uanzishwaji wa Halmashauri hiyo mpya ya Butiama kwa Kaimu Mkurugenzi Richard Mihayo alisema kuwa Halmashauri ya Musoma ina eneo kubwa hivyo inahitaji kupata majimbo mengine mawili.



 “Changamoto zilizokuwa zinaikabili Halmashauri hii ni ukubwa wa eneo na hapa tumeanza tu kugawa katika Halmashauri mbili lakini inatakiwa iwe na majimbo aidha matatu ya uchaguzi ili kuweza kuwaqfikishia huduma wananchi wa maeneo hao,” alisema Tuppa.



 Alisema kuwa pamoja na hilo viongozi wa Halmashauri hizo waache utendaji kazi wa mazoea ili waweze kuwatendea haki wananchi wao ikiwa pamoja na kuwatatulia kero mbalimbali zinazowakabili.



 Ugawaji wa Halmashauri hizo ilifanyika ikiwa ni pamoja na kugawana raslimali na madeni yaliyokuwepo katika Halmashauri hiyo hatua hiyo ambayo ilikwisha kwa amani na utulivu huku kila mjumbe akiridhia ugawaji huo.



 Hivi karibuni katika mchakato kama huo wa kugawa Halmashauri ya Tarime na Halmashauri ya Mji wa Tarime vurugu zilitokea kutokana na madiwani watatu wa viti maalumu wa CCM na Chadema kukataliwa kuingiwa Mjini kwa madai hawakai maeneo ya mjini na kusababisha kutoelewana na madiwani kurushia maneno na kuvunjiaka bila muafa.



 MWISHO











 Na Thomas Dominick

 Butiama.



 HALMASHARI ya Wilaya ya Musoma Mkoa wa Mara imejikuta katika wakati mgumu pale baada ya madiwani kuitaka halmashauri kutoa ufafanuzi wa kina juu ya malimbikizo ya madeni kubwa la Milioni 402 ambazo zimeweza kusababisha kuzorota kwa  suala zima la Maendeleo kwa wananchi.



 Wakichangia hoja mbalimbali hii leo katika  kikao maalum kilichokuwa na lengo la kujadili mgawanyiko wa rasirimali kati ya halmashauri ya wilayaya  Musoma pamoja na Butiama, Diwani wa kata ya Nyambono Grayson Mfungo amesema kuwa  malimbikizo ya milioni 402 ni mzigo mkubwa kwa Halmashauri kitendo ambacho kinaweza kukwamisha baadhi ya shuguli za kimaendeleo.



 Kambi ya upinzani walitaka kujua halmashauri ilikuwa wapi mpaka

 inafikia hatua ya malimbikizo kwa watendaji  wanaokaimu idara mbali mbali na kudai kuwa watakubaliana  na mgawanyiko wa raslimali endapo tu halmashauri itatoa majibu ya kuridhisha kuhusiana na suala hili.



 Akijibu hoja hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Musoma Fidelica Myovela, alikiri kuwa  halmashauri inakabiliwa na deni kubwa na sehemu kubwa ya deni hilo nikutokana na posho za kukaimu nafasi ya Ukuu wa Idara  ambapo zilistahili kulipwa kwa wakuu mbalimbali wa idara.



 Naye Mkuu wa Mkoa wa huo,  John Tuppa  alikiri kupokea taarifa za malimbikizo ya madeni na  amehaidi kulipeleka suala hilo katika

 serikari kuu sambamba na uwasilishwaji wa wakuu mbali mbali wa idara ili kuweza kuondokana na tatizo la ukaimu ambapo limekuwa

 likisababisha mzigo mkubwa Kwa halmashauri.



 Aidha alizitaka halmashauri  kuhakikisha kuwa zinaboresha  mapato yake ya ndani na kuziba mianya yote inayopita fedha hizo katika mifuko ya watu binafsi ili  kuepuka ongezeko la msaada wa kifedha kutoka serikali kuu.



 “Viongozi wanashindwa kusimamia sheria za ukusanyaji mapato na hicho ndicho chanzo cha upotevu wa mapato ya ndani utakuta viongozi wana vitabu bandia vya risti za kukusanyia fedha za serikali, viongozi kama hawa hawatufai,”alisema Tuppa.



 Halmashauri ya wilaya ya Musoma imeweza kujitenga rasmi na kuzaa wilaya mbili  Butiama pamoja na Musoma Vijijini inayopigiwa debe iitwe kwa jina Nyanja lengo kuu likiwa kurahisisha huduma kwa wananchi.





 MWISHO


Read More...

Saturday, August 17, 2013

SERIKALI YATANGAZA NEEMA KWA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI WA BUHEMBA WILAYA YA BUTIAMA MKOA WA MARA






 Baadhi ya viongozi waliohudhuria kikao cha kutangaziwa neema kwa wachimbaji wadogo wa madini wa Buhemba Wilaya ya Butiama Mkoa wa Mara katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya Angeline Mabula.
Mkuu wa Wilaya ya Butiama Angeline Mabula akizungumza na viongozi na waandishi wa Habari hawapo pichani juu ya serikali kutenga maeneo kwa wachimbaji wadogo wa madini wa Buhemba.

Na Thomas Dominick,
Butiama.

SERIKALI imeshatimiza ndoto za wachimbaji wadogo baada ya kutangaza kukamilisha kazi ya upimaji wa viwanja 35 venye ukubwa wa hekta 9.64 katika eneo la Rwabasi na Mirwa katika machimbo ya Buhema Mkoani Mara.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari wilayani humo, Mkuu wa wilaya Angeline Mabula alisema kuwa utengaji wa maeneo hayo ni baada ya hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo kwenye bunge la bajeti 2013/14 kuwa wachimbaji hao wanatengewa maeneo rasmi ya uchimbaji.

“Kutokana na ari kubwa ya watafutaji wakubwa wa madini kuchukua leseni katika wilaya ya Butiama kumekuweko na uhaba wa maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo, Hali hii ilizua malalamiko kutoka kwa wachimbaji hao ambao waliomba kutengewa maeneo rasmi ya uchimbaji katika eneo la Buhemba,”alisema Mabula.

Alisema kuwa kabla ya upimaji huo eneo hilo lilifanyiwa uchunguzi wa Kijiolojia, Kijiofizikia na Kijiokemia na wataalamu kutoka wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) kubaini kuwa eneo hilo lina miamba yenye dhahabu,”alisema.

Alisema kuwa zoezi hilo la upimaji lilikuwa shirikishi likihusisha wachimbaji na viongozi wa kata ya Buhemba na Mirwa ambapo kukamilika kwa zoezi hilo alitoa wito kwa wananchi wa Kata za Buhemba na Mirwa kutumia fursa hiyo vizuri kutuma maombi ya leseni kwa afisa madini mkazi wa Musoma kupitia vikundi vyao ushirika.

Pia aliwaagiza maafisa madini kuhakikisha kuwa leseni zinatayarishwa mapema kwa wale wote watakaoomba na wahusika wanaonyeshwa maeneo ya leseni zao kwa wakati, Pia alitoa wito kwa wachimbaji wadogo kujiepusha kabisa vitendo vya uvamizi wa maeneo yanayomilikiwa na watu wengine au mwekezaji, hususani eneo la STAMICO na mwekezaji Manjaro Resources ya nchini Australia.

Mabula aliwaomba wananchi wawe wavumilivu na watii wa sheria bila shurti hasa pale wanapokuwa na malalamiko kwa utatuzi wa kero zao unazingatiwa kwa kufuata sheria za nchi, ambapo pia aliahidi kuwa ofisi yake kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini kuendelea kuwatafutia wananchi maeneo zaidi ya uchimbaji.

Naye Kaminishi Msaidizi Madini Kanda ya Ziwa Salim Said Salim alisema kuwa ofisi yake itahakikisha wachimbaji wadogo wanapata leseni za madini ndani ya wiki moja bila kuwa na usumbufu wowote.

MWISHO
Read More...

KIAMA CHATANGAZWA KWA WATENDAJI KATA NA VIJIJI, WAKULIMA NA WACHOMA MKAA WA WILAYA YA BUTIAMA MKOA WA MARA.







 Hii ni sanamu ya baba wa Taifa iliyowekwa nje ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Butiama.
 Mkuu wa Wilaya ya Butiama akizungumza jambo fulani na waandishi wa habari ofisini kwake.

Na Thomas Dominick,

Butiama



WATENDAJI wa Kata na Vijiji Wilaya ya Butiama, Mkoa wa Mara kukiona cha moto endapo wataendelea kuwaruhusu wananchi wao kulima maeneo oevu na wanaoendelea kukata miti ovyo na kuharibu mazingira ambayo itasababisha jangwa.



Kauli hiyoi ilitolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Angeline Mabula wakati akifungua kikao ca Ushauri cha Wilaya (DCC) kwa kilichoitishwa kwa ajili ya kujadili ugawaji wa raslimali na madeni ya Halmashauri ya Musoma kutokana na kuigawa Halmashauri hiyo katika wilaya mbili ya Butiama na Musoma ambapo inapigiwa debe iitwe wilaya ya Nyanja.



Mabula alisema kuwa wananchi wa wilaya ya Butiama wamekuwa wakilima maeneo oevu na kusababisha ukame ambao unatishia maisha ya viumbe hai pamoja na binadamu wanaoishi kuzunguka maeneo hayo.



“Nitafanya ziara kupitia sehemu mbalimbali kukagua maeneo oevu na nikikuta wananchi wanalima sitahangaika na mkulima huyo bali badala yake nitaanguka na mtendaji wa eneo hilo kwani atakuwa ameshindwa kutekeleza sheria za mazingira,”alisema Mabula.



Pia alisema kuwa wilaya hiyo inaongoza kwa kukata miti na kuchoma mkaa ambapo pia aliahidi kufanya oparesheni hivi karibuni ya kuwakamata wauza mkaa wanaotokea wilaya hiyo na akihojiwa na kusema kata anayotoka atachukuliwa hatua yeye na mtendaji wa eneo hilo ambapo watapelekwa kwenye vyombo vya sheria sambamba na kuwashitaki.



Baada ya tamko la Mkuu wa wilaya wajumbe waliokuwepo katika mkutano huo waliguna kwa pamoja ndipo alipoamua kukazia usemi wake, “ Nyie mgune tu lakini nitakapopita maeneo yenu na kufanya opresheni hiyo ndipo mtakapojua nini nakimaanisha sitanii kwa hili,”alisema.



Ndipo alipomuagiza Mkurugenzi wa wilaya hiyo Fidelica Myovela kuhakikisha anatenga maeneo maalumu kwa ajili ya kukata miti na kuchoma mkaa na sio kila eneo lenye miti litumike kwa shughuli hiyo. 

Mwisho.
Read More...

Thursday, August 15, 2013

MKUU WA WILAYA YA BUTIAMA MKOA WA MARA AWATIMUA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA KWENYE KIKAO CHA USHAURI WA WILAYA (DCC)







 MKUU WA WILAYA YA BUTIAMA ANGELINA MABULA AKIWA OFISINI KWAKE (PICHA KUTOKA MAKTABA YA BLOG)


Na Thomas Dominick,
Musoma.

MKUU wa Wilaya ya Butiama Mkoa wa Mara Angelina Mabula amewafukuza viongozi wa vyama vya siasa kwenye kikao cha Ushauri cha Wilaya hiyo (DCC) baada ya wajumbe kuibua vurugu kubwa na kuwataka viongozi hao ambao vyama vyao havipo wilayani humo kuondolewa kwenye kikao hicho.

Kikao hicho kilichoanza kwa wajumbe kutoka kwenye baadhi ya vyama vya upinzani kumuomba Mkurugenzi Fidelica Myovela kuwaondoa viongozi hao ambao aliwapa mialiko kinyemelea wakati hawafanyi kazi katika wilaya hiyo.

“Wakulaumiwa ni wewe Mkurugenzi kutokana na utaratibu wako mbovu uliotumia kuwaalika viongozi ambao sio wa Butiama na hawana ofisi katika wilaya yetu hawa wote ni viongozi wa Manispaa ya Musoma,”alisema    Richard Choge Katibu wa Chadema wilaya hiyo.

Baada ya shutuma hizo kwa Mkurugenzi ndipo Mkuu wa Wilaya kabla ya kufungua kikao hicho alitoa tamko zito  la kuwataka kuondoka ndani ya ukumbi huo viongozi hao ambao hawana ofisi wilayani humo.

“Sitaki vurugu kwenye kikao change hivyo nawaomba wale ambao hawausiki na wilaya yetu watoke nje mara moja kabla sijawatoa kwa nguvu sipendi tuanze vibaya,”alisema Mabula.

Baada ya tamku hilo Kamanda wa Polisi wa Wilaya hiyo Audax Majaliwa aliingilia kati na kuwatoa nje huku akiomba askari kwa ajili ya ulinzi ambapo baada ya dakika kadhaa askari waliongezeka na kuzunguka ukumbi huo na hali kurudi kuwa shwari na kuendelea na kikao.

Vyama ambavyo viongozi wake walifukuzwa ni pamoja na UDP, NLD, NCCR Mageuzi, TADEA,ADCDEMOKRASIA MAKINI na SAU ambavyo vyote havia ofisi ndani ya wilaya hiyo.

Akifungua kikao hicho Mabula aliwataka wajumbe kutumia nafasi hiyo kutoa ushauri bora ambao utakwenda kwenye kikao cha Ushauri wa Mkoa (RCC) ili kupata Baraka ama kuhalalishwa na kuwa taarifa kamili ya wilaya na mkoa kwa jumla.

Katika taarifa yake alisema kuwa wilaya hiyo inatakiwa kugawanywa kwa rasilimali na madeni ya halmashauri ya Musoma ambayo itavunjwa rasmi Augosti 20 mwaka huu na kuwaomba kuwa usikivu wao katika kupitia taarifa mara itakapowasilishwa ili iwe manufaa kwa wana butiama.

“Ndugu wajumbe ni imani yangu kuwa mtatumia nafasi hii vizuri katika kufikia ushauri wenye tija, mtakuwa na nafasi nzuri ya kutafakari kwa kina kwa manufaa ya wote aidha mtatoa ushauri wenye tija ukizingatia kuwa pamoja na halmashauri kugawanywa bado halmashauri zote mbili zitaendelea kuwa chini ya wilaya ya Butiama,”alisema.

Aliongeza kuwa lengo la kugawa halmashauri hiyo ni kusogeza huduma kwa wananchi  pia yawezekana kuwa njia ya baadaye kupata wilaya inayojitegemea mwenendo mzimahuo ni kwa ajili ya kuijenga na kuiimarisha wilaya katika mustakabali wa kumuenzi muasisi wa Taifa hilo Hayati Mwl. Julius Nyerere ambaye amepewa heshima kubwa.   

MWISHO.
Read More...

Saturday, August 10, 2013

PEACE MAKER YAUA DEREVA WA GARI DOGO PAPO HAPO MUSOMA MKOANI MARA BAADA YA GARI DOGO HIYO KUINGIA UVUNGUNI

 WANANCHI WAKICHUNGULIA GARI DOGO AMBALO LIPO CHINI YA BASI HILO BAADA YA KUINGIA UVUNGUNI AMBAPO DEREVA WA GARI DOGO KUFA PAPO HAPO ENEO LA MARA OIL WILAYANI MUSOMA MKOA WA MARA AJALI HII ILITOKEA SIKU YA IDD ASUBUHI.


 HIVI NDIVYO GARI DOGO LIKIWA UVUNGUNI MWA PEACE MAKER




Read More...