MKUU WA WILAYA YA BUTIAMA ANGELINA MABULA AKIWA OFISINI KWAKE (PICHA KUTOKA MAKTABA YA BLOG)
Na Thomas Dominick,
Musoma.
MKUU wa Wilaya ya Butiama Mkoa wa Mara Angelina Mabula
amewafukuza viongozi wa vyama vya siasa kwenye kikao cha Ushauri cha Wilaya
hiyo (DCC) baada ya wajumbe kuibua vurugu kubwa na kuwataka viongozi hao ambao
vyama vyao havipo wilayani humo kuondolewa kwenye kikao hicho.
Kikao hicho kilichoanza kwa wajumbe kutoka kwenye baadhi ya
vyama vya upinzani kumuomba Mkurugenzi Fidelica Myovela kuwaondoa viongozi hao
ambao aliwapa mialiko kinyemelea wakati hawafanyi kazi katika wilaya hiyo.
“Wakulaumiwa ni wewe Mkurugenzi kutokana na utaratibu wako
mbovu uliotumia kuwaalika viongozi ambao sio wa Butiama na hawana ofisi katika
wilaya yetu hawa wote ni viongozi wa Manispaa ya Musoma,”alisema Richard Choge Katibu wa Chadema wilaya
hiyo.
Baada ya shutuma hizo kwa Mkurugenzi ndipo Mkuu wa Wilaya
kabla ya kufungua kikao hicho alitoa tamko zito
la kuwataka kuondoka ndani ya ukumbi huo viongozi hao ambao hawana ofisi
wilayani humo.
“Sitaki vurugu kwenye kikao change hivyo nawaomba wale ambao
hawausiki na wilaya yetu watoke nje mara moja kabla sijawatoa kwa nguvu sipendi
tuanze vibaya,”alisema Mabula.
Baada ya tamku hilo Kamanda wa Polisi wa Wilaya hiyo Audax
Majaliwa aliingilia kati na kuwatoa nje huku akiomba askari kwa ajili ya ulinzi
ambapo baada ya dakika kadhaa askari waliongezeka na kuzunguka ukumbi huo na
hali kurudi kuwa shwari na kuendelea na kikao.
Vyama ambavyo viongozi wake walifukuzwa ni pamoja na UDP,
NLD, NCCR Mageuzi, TADEA,ADCDEMOKRASIA MAKINI na SAU ambavyo vyote havia ofisi
ndani ya wilaya hiyo.
Akifungua kikao hicho Mabula aliwataka wajumbe kutumia
nafasi hiyo kutoa ushauri bora ambao utakwenda kwenye kikao cha Ushauri wa Mkoa
(RCC) ili kupata Baraka ama kuhalalishwa na kuwa taarifa kamili ya wilaya na
mkoa kwa jumla.
Katika taarifa yake alisema kuwa wilaya hiyo inatakiwa
kugawanywa kwa rasilimali na madeni ya halmashauri ya Musoma ambayo itavunjwa
rasmi Augosti 20 mwaka huu na kuwaomba kuwa usikivu wao katika kupitia taarifa
mara itakapowasilishwa ili iwe manufaa kwa wana butiama.
“Ndugu wajumbe ni imani yangu kuwa mtatumia nafasi hii
vizuri katika kufikia ushauri wenye tija, mtakuwa na nafasi nzuri ya kutafakari
kwa kina kwa manufaa ya wote aidha mtatoa ushauri wenye tija ukizingatia kuwa
pamoja na halmashauri kugawanywa bado halmashauri zote mbili zitaendelea kuwa
chini ya wilaya ya Butiama,”alisema.
Aliongeza kuwa lengo la kugawa halmashauri hiyo ni kusogeza
huduma kwa wananchi pia yawezekana kuwa
njia ya baadaye kupata wilaya inayojitegemea mwenendo mzimahuo ni kwa ajili ya
kuijenga na kuiimarisha wilaya katika mustakabali wa kumuenzi muasisi wa Taifa
hilo Hayati Mwl. Julius Nyerere ambaye amepewa heshima kubwa.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment