Mkuu wa Wilaya ya Butiama akizungumza jambo fulani na waandishi wa habari ofisini kwake.
Na Thomas Dominick,
Butiama
WATENDAJI wa Kata na Vijiji Wilaya ya Butiama, Mkoa wa Mara kukiona
cha moto endapo wataendelea kuwaruhusu wananchi wao kulima maeneo oevu na
wanaoendelea kukata miti ovyo na kuharibu mazingira ambayo itasababisha jangwa.
Kauli hiyoi ilitolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Angeline
Mabula wakati akifungua kikao ca Ushauri cha Wilaya (DCC) kwa kilichoitishwa
kwa ajili ya kujadili ugawaji wa raslimali na madeni ya Halmashauri ya Musoma kutokana
na kuigawa Halmashauri hiyo katika wilaya mbili ya Butiama na Musoma ambapo
inapigiwa debe iitwe wilaya ya Nyanja.
Mabula alisema kuwa wananchi wa wilaya ya Butiama wamekuwa
wakilima maeneo oevu na kusababisha ukame ambao unatishia maisha ya viumbe hai
pamoja na binadamu wanaoishi kuzunguka maeneo hayo.
“Nitafanya ziara kupitia sehemu mbalimbali kukagua maeneo
oevu na nikikuta wananchi wanalima sitahangaika na mkulima huyo bali badala
yake nitaanguka na mtendaji wa eneo hilo kwani atakuwa ameshindwa kutekeleza
sheria za mazingira,”alisema Mabula.
Pia alisema kuwa wilaya hiyo inaongoza kwa kukata miti na
kuchoma mkaa ambapo pia aliahidi kufanya oparesheni hivi karibuni ya kuwakamata
wauza mkaa wanaotokea wilaya hiyo na akihojiwa na kusema kata anayotoka
atachukuliwa hatua yeye na mtendaji wa eneo hilo ambapo watapelekwa kwenye
vyombo vya sheria sambamba na kuwashitaki.
Baada ya tamko la Mkuu wa wilaya wajumbe waliokuwepo katika
mkutano huo waliguna kwa pamoja ndipo alipoamua kukazia usemi wake, “ Nyie
mgune tu lakini nitakapopita maeneo yenu na kufanya opresheni hiyo ndipo mtakapojua
nini nakimaanisha sitanii kwa hili,”alisema.
Ndipo alipomuagiza Mkurugenzi wa wilaya hiyo Fidelica
Myovela kuhakikisha anatenga maeneo maalumu kwa ajili ya kukata miti na kuchoma
mkaa na sio kila eneo lenye miti litumike kwa shughuli hiyo.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment