Monday, December 3, 2012

MAADHIMISHO YA SIKU YA WATU WENYE ULEMAVU KITAIFA YAFANYIKA MKOANI MARA


 Mkuu wa mkoa wa Mara John Tuppa aliyemwakilisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipokea maelezo wakati akikagua kazi za watu wenye ulemavu katika maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu yaliyofanyika katika uwanja wa Karume Manispaa ya Musoma.
 Watu wenye ulemavu wakipita mbele ya mgeni Rasmi Mkuu wa mkoa wa Mara John Tuppa katika maadhimisho ya siku watu wenye ulemavu yaliyofanyika katika uwanja wa Karume Manispaa ya Musoma.
Kila mtoto ana haki ya kucheza ndivyo bango linavyosomeka ambalo limebebwa na wanafunzi wakipita mbele Mkuu wa mkoa wa Mara John Tuppa katika maadhimisho ya siku ya  watu wenye ulemavu yaliyofanyika katika uwanja wa Karume Manispaa ya Musoma.
 Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mwembeni wakipita mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tuppa katika  maadhimisho siku ya watu wenye ulemavu yaliyofanyika katika uwanja wa Karume Manispaa ya Musoma.
 Kijana Mlemavu wa mikono akiandika kwa kutumia miguu katika maadhimisho siku ya watu wenye ulemavu yaliyofanyika katika uwanja wa Karume Manispaa ya Musoma.
 Mkalimani wa Viziwi akiwatafusiria Viziwi hotuba ya mgeni mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tuppa katika  maadhimisho siku ya watu wenye ulemavu yaliyofanyika katika uwanja wa Karume Manispaa ya Musoma.
 Mlemavu Victoria akipokea zawadi ya mshindi wa kwanza katika mbio za baiskeli toka kwa Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tuppa katika  maadhimisho siku ya watu wenye ulemavu yaliyofanyika katika uwanja waKarume.
 Zawadi maalumu iliyotolewa kwa aliyekuwa mgeni rasmi Waziri Mkuu Mizengo Pinda toka katika chama cha Walemavu iliyopokelewa na mwakilishi wake Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tuppa katika  maadhimisho siku ya watu wenye ulemavu yaliyofanyika katika uwanja wa Karume.

Na Thomas Dominick,
Musoma

SERIKALI imeagiza Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri za miji, Wilaya
na mawakala zinazotoa huduma kwa watu wenye ulemavu kuweka mipango madhubuti ya haki za watu wenye ulemavu kuimarisha kuimarisha mahusiano yaliyopo kati ya vyama vya watu wenye ulemavu na watendaji.

Akisoma hotuba ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda Mkuu wa Mkoa wa Mara John
Tuppa Siku ya maadhimisho ya watu wenye ulemavu Duniani ambapo kitaifa ilifanyika Mkoani hapo, alisema kuwa serikali kuu inaendelea kutangua madaraka kwenda ngazi ya serikali za mitaa ili kusogeza huduma za ustawi wa jamii.

“Hatua hii itawezesha Halmashauri zote nchini kusimamia na kutekeleza
huduma za watu wenye ulemavu, hivyo serikali, asasi zisizo za kiserikali na watu binafsi zishiriki katika kuhakikisha kwamba juhudi za makusudi zinafanywa ili kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu,”alisema Tuppa.

Alisema kuwa serikali itaendelea kusimamia upatikanaji wa taarifa za
  mifumo isiyo rasmi kwa watu wenye ulemavu hususani viziwi kwa kuhakikisha kuwa katika vyombo vya habari kupitia luninga kuhakikisha mkalimani wa lugha za alama ili waweze kupata taarifa muhimu zinazotolewa kwa manufaa ya maendeleo ya nchi na ustawi wa jamii kwa ujumla.

“Serikali itaendelea kuboresha miundo mbinu kwa watu wenye ulemavu
  ikiwa ni majengo yanayotoa huduma kwa umma kutofikika na kusababisha walemavu kushindwa kupata huduma muafaka na wanazostahili,”alisema.

Alisema kuwa Serikali kupitia kitengo cha michoro na ramani wameandaa
mwongozo wa ramani za majengo ya umma hivyo kabla ya kufanya ujenzi wowote lazima ramani ikaguliwe ili kuona kama imekidhi mahitaji hayo.

Tuppa alisema kuwa Serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii
inatenga fedha kila mwaka ili kuviongezea uwezo vyama hivyo na suala la kutotosheleza kwa ruzuku linatokana na uwezo wa serikali kifedha na majukumu yanayohusiana na huduma katika sekta mbalimbali.

Alisema kuwa suala la watu wenye ulemavu ni mtambuka ambalo linamgusa
kila mmoja na kila wizara inatakiwa kuwa na dawati la kuratibu masuala la watu wenye ulemavu kwa kushitikiana pamoja na wizara ya afya na ustawi wa jamii yenye dhamana juu ya masuala ya watu wenye ulemavu nchini.
 
MWISHO

0 comments:

Post a Comment