Wednesday, June 5, 2013

KAMPUNI YA AFRICAN BARRICK GOLD NORTH MARA WAKABIDHI HUNDI YA M. 10 KWA MWANDAAJI WA REDD'S MISS MARA 2013




 Washiriki wa Redd's Miss Mara wakiwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara wakisubiri kushuhudia ukabidhiwa kwa hundi ya M.10 kutoka Kampuni ya Madini ya African Barrick Gold North Mara.
 Kaimu Katibu Tawala Joseph Makingaakipokea hundi toka kwa Mratibu wa Huduma za jamii wa Kampuni ya Madini ya African Barrick Gold North Mara Fatuma Msumi.
 Kaimu Katibu Tawala Joseph Makingaakimkabidhi Mkurugenzi wa Homeland Intertainment and Promotion Godson Mkama
 Waandishi wa habari wakifanya mahojiano na washiriki wa Redd's miss Mara 2013.
 Waandishi wa habari wakifanya mahojiano na washiriki wa Redd's miss Mara 2013.
 Mkurugenzi wa Homeland Intertainment and Promotion Godson Mkama akifanya mahojiano na waandishi wa habari.
Washiriki wa Redd's Miss Mara wakiwa katika picha ya pamoja.



Na Thomas Dominick,
Musoma

Kampuni ya Madini ya African Barrick Gold North Mara umekabidhi fedha shilingi M. 10 kwa ajili ya ufadhili wake wa shindano la Redd's Miss Mara 2013.

Fedha hizo zilikabidhiwa mbele ya Kaimu Katibu Tawala Joseph Makinga na mbele ya waandishi wa habari wa Mkoa huo.

Makinga aliomba kampuni hiyo kuongeza udhamini mwakani ili mkoa uweze kufanya vizuri katika mashindano hayo kila mwaka pamoja na Chuo cha Musoma utalii kuongeza idadi ya washiriki wanaosoma katika chuo hicho toka watat hadi kumi.

Akikabidhi fedha hizo Mratibu wa Huduma za Jamii kutoka kwenye kampuni hiyo, Fatuma Msumi alisema kuwa wameamua kufadhili mashindano hayo tangu 2006 kwa ajili ya kurudisha fedha kwa jamii ya mkoa huo.

"Sisi tumekuwa tunatoa fedha kwa jamii kupitia miradi mbalimbali lakini kwa hili tumeamua kutoa fedha kupitia vipaji vyao ili kuwapatia uwezo wa kushinda katika mashindano makubwa ya kitaifa na dunia pia,"alisema.

Mwandaaji wa shindano hilo ambaye ni Mkurugenzi wa Home land Intertainment and Promotion, Godson Mkama ameshukuru kampuni hiyo kutoa kiasi hicho cha fedha na kusema kuwa wamejiandaa vyema kuhakikisha mshindi wa mwaka huu anauwakilisha mkoa huo vizuri.

"Lengo letu ni kufanya vizuri zaidi mwaka huu kuhakikisha tunashika nafasi ya kwanza redd's Miss Lake zone na Redd's Miss Tanzania,"alisema Mkama.

Washindani hao pia walisema kuwa shindano la mwaka huu ni gumu kutokana na washiriki wake kuwa ni warembo na wanajiamini kuliko miaka ya nyuma.

"Ninachoweza kusema kuwa shindano la mwaka huu ni gumu sana ukizingatia kila mshiriki amejiandaa vizuri sana na tunavutia mbele ya watu,"alisema Lilian Josephat mshiriki toka Wilaya ya Butiama.

MWISHO.



0 comments:

Post a Comment