Tuesday, June 18, 2013

MAKILAGI CUP YAFUNGWA RASMI KATIKA KATA YA BWERI MANISPAA YA MUSOMA MKOANI MARA

 Katibu wa Umoja wa Vijana Wilaya ya (UVCCM)  Musoma Mjini Khalid King akiwa na Mfadhili ya Michuano ya Makilagi Cup ambaye ni Mbunge wa viti Maalum (CCM) Amina Makilagi wakiangalia fainali ya Ligi hiyo kati ya Machinjioni FC na Majengo FC ambao majengo FC waliibuka washindi kwa magoli 4-3 katika uwanja wa shule ya Sekondari ya Morembe. 
 Mbunge wa viti Maalum (CCM) Amina Makilagi akizungumza na timu ashindi na shiriki hawapo pichani kuhusu michuano hiyo na adhima yake ya kuboresha maisha ya vijana hao kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya kujishughulisha katika kuinua kipato chao kwa kuanzisha vikundi vya ujasiliamali.
 Mbunge wa viti Maalum (CCM) Amina Makilagi akinyanyua Kombe juu kabla ya kuikabidhi timu bingwa ya majengo FC.
 Mbunge wa viti Maalum (CCM) Amina Makilagi akiwavisha medali wachezaji wa majengo FC ambayo ndio timu bingwa wa michuano ya Makilagi Cup.
 Timu ya Majengo FC wakiwa katika picha ya Pamoja huku kombe lao likiwa mbele.
 Mbunge wa viti Maalum (CCM) Amina Makilagi akikabidhi kombe kwa timu kapteni na kocha wa timu ya majengo FC.



Na Thomas Dominick,
Musoma

MASHINDANO ya Mpira wa miguu yaliyodhaminiwa na Mbunge wa Viti Maalumu  (CCM) na Katibu UWT Taifa Amina Makilagi yanayojulikana kama Makilagi Cup yamefika mwisho baada ya timu ya Majengo FC kuibuka washindi katika fainali iliyowakutanisha na timu ya Machinjioni FC zote za kata ya Bweri Manispaa ya Musoma Mkoa wa Mara.

Mchezo huo ulioanza majira ya saa kumi jioni katika viwanja vya shule
ya sekondari ya kutwa Molembe iliyopo katika kata ilishuhudiwa timu ya majengo FC wakiibamiza timu ya Machinjioni FC kwa magoli 4-3 katikia mchezo wa vuta nikuvute.

Wafungaji wa timu ya Majengo FC walikuwa ni Yohana Mirobo aliyefunga magoli mawili na Nyanda Rubeni naye aliyefunga magili mawili, na kwa upande wa machinjioni Fc magoli yalifungwa na Vicent Magesa, Adamu kulenga, Alex Andrew huku Vicent magesa akikosa penaiti dakika ya 89.

Baada ya mchezo huo Makilagi alikabidhi zawadi mbalimbali kwa
washiriki wa michuano hiyo ambapo timu ya nne na ya sita walizawadiwa pesa tasilimu sh. 50,000/=, timu yenye nidhamu ambayo ni Bweri FC walipata 50,000/=.

Mshindi wa tatu ambaye ilikuwa timu ya Victoria FC alizawadiwa sh.
200,000/=, mshindi wa pili mchinjioni FC walipata sh. 300,000/= na
mshindi wa kwanza ambaye ni Majengo FC walipata Kikombe, medali pamoja na fedha sh. 500,000/=.

Akifunga mashindano hayo Makilagi aliwaomba vijana hao wajiunge katika vikundi ili waweze kupata fedha kwa ajili ya kuanzisha miradi ya
maendeleo ambapo itawasaidia kukuza uchumi wao na wa Taifa.

"Mimi kama Mbunge ambaye nimetokea katika kata hii nimevutiwa sana na ninaguswa na matatizo yanayowakabili vijana hasa katika ajira na michezo hii imefungua ukurasa mpya kwenu nawaomba vijana wote mjiunge katika vikundi ili tuweze kuwasaidia kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali,"alisema makilagi.

Makilagi alisema kuwa ligi hiyo itakuwa ikichezwa kila baada ya miezi
sita huku shughuli za maendeleo kwa vijana hao zikiendelea kama
alivyowaahidi kuwa atawatafutia fedha kwa ajili ya maombi yao
waliyotoa kwa mbunge huyo.




Mwisho

0 comments:

Post a Comment