Tuesday, November 27, 2012

JESHI LA POLISI LAVAMIA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA





Wanaharakati wa kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake wakiwa na mabango kwa ajili ya kuanza maandamano katika kampeni ya siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake iliyofanyika katika Kijiji cha Kitasakwa Kata ya Bwiregi Wilayani Butiama iliyoandaliwa na Shirika la kutetea Haki za Wanawake na Watoto la ABCFoundation Chini ya Ufadhiri wa Shirika la (WILDAF).
 Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma akipokea maandamano (hawapo Pichani) katika kampeni ya siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake iliyofanyika katika Kijiji cha Kitasakwa Kata ya Bwiregi Wilayani Butiama.

Na Thomas Dominick,
Butiama,

JUMLA ya matukio 201 ya ukatili wa Kijinsia yamelipotiwa katika Jeshi la Polisi Mkoani Mara kutokea  maeneo mbalimbali ya Mkoa huo katika kipindi cha mwezi Januari hadi Novemba Mwaka huu huku jamii ikitakiwa kubadilika na kukomesha matukio ya namna hiyo kuendelea kutokea katika Jamii.

Kauli hiyo ilitolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani Mara Kamishina
Msaidizi Mwandamizi Absalom Mwakyoma alipokuwa akifungua kampeni ya siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake iliyofanyika katika Kijiji cha Kitasakwa Kata ya Bwiregi Wilayani Butiama iliyoandaliwa na Shirika la kutetea Haki za Wanawake na Watoto la ABC Foundation Chini ya Ufadhiri wa Shirika la (WILDAF).

Alisema idadi hiyo imeongezeka tofauti na mwaka uliopita ambapo katika kipindi cha Mwaka jana matukio ya ukatili yaliyolipotiwa yalikuwa 148 huku watuhumiwa 51 walifikishwa Mahakamani na kati ya hao watuhumiwa 10 tayari wamekwisha hukumiwa na wanatumikia adhabu zao gerezani.

Alidai Mwanamke ni mtu ambaye anachangia kwa kiasi kikubwa katika Maendeleo ya Kijamii ikiwemo kuchangia shughuli za Kiuchumi katika Jamii pamoja na kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza Elimu kwa Watoto kwa kuwa wao kwa asilimia kubwa ndio wanaokuwa nao karibu hivyo anastahili kuheshimiwa na kupewa haki stahili.

Kamanda Mwakyoma alieleza kuwa Binadamu wote ni sawa na wanastahili kutambuliwa na kuheshimiwa utu wao hivyo ni wazi kwamba watu wote hususani Wanawake ambao wamekuwa wakinyanyaswa kutokana na jinsia zao ni ukiukwaji wa katiba ya Nchi na misingi ya Haki za Binadamu pale wanapofanyiwa ukatili.

Alisema Jeshi la Polisi kupitia dawati la jinsia kwa kushirikiana na
Asasi mbalimbali zinazopambana na masuala ya ukatili wa kijinsia
watahakikisha mapambano ya kukomesha ukatili wa kijinsia Mkoani Mara yanakomeshwa hususani kwa Wanawake na Watoto wanaofanyiwa Ukeketaji.

“Nimeajiliwa kwa kufanya kazi na nitahakikisha nawashughulikia kwa mujibu wa Sheria wale wote ambao bado wanaendeleza matukio ya unyanyasaji kwa Wanawake na Watoto pale watakapobainika na sasa ni wajibu wa kila Mwananchi kubadilika na kuachana na masuala hayo.

“Lazima Mwanamke aheshimiwe na kila mmoja tusione ajabu leo kumuona Kamanda wa Polisi akiwa mgeni rasmi katika uzinduzi huu kwa maana sasa tumeamua kwa dhati kushirikiana na jamii katika masuala yote likiwemo suala la kupinga na kukomesha unyanyasaji wa kijinsia na ndio iliyopelekea Mwaka 2007 ukaanzishwa mtandao wa Polisi Wanawake na baadae Mwaka 2009 likaanzishwa dawati la jinsia la Wanawake na Watoto,”alisema Kamanda Mwakyoma.

Awali katika uzinduzi huo wa siku 16 za kupinga ukatili wa
Kijinsia,Mkuu wa Wilaya ya Butiama Angelina Mabula aliwataka Wanawake kutokuogopa kutoa taarifa zinazohusiana na masuala ya ukatili wa Kijinsia ili kila mmoja anaye husika aweze kufikishwa katika vyombo vya Sheria ili hatua dhidi yao ziweze kuchukuliwa.

Alisema inahitajika mikakati madhubuti zaidi kwa lengo la kuondoa
masuala ya ukatili wa kijinsia kwani pamoja na kuwepo Sheria za kuzuia masuala ya ukatili bado kumekuwepo na matukio kama hayo na kuwa kikwazo katika Maendeleo ya Wanawake.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la ABC Foundation, Eustance Nyarugenda alilishukuru Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF) Kupitia Shirika la Kivulini kwa  ufadhiri wa siku hizo 16 za kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na kuahidi kuendelea na mapambano dhidi ua ukatili hata baada ya kumalizika kwa siku hizo.
Read More...

Monday, November 26, 2012

UZINDUZI WA MOTO WA NYIKA WAFUNIKA MKOANI MARA

 Naibu Meya Bwire Nyamwero akionyeshwa moja ya mabanda ya kuhifadhia kuku lililotengenezwa na Vijana wajasiriamali wa Shule ya Ufundi ya Musoma Mkoani Mara 
 Naibu Meya Bwire Nyamwero akizungumza jambo na wajasiriamali walioleta bidhaa zao kwa ajili ya maonyesho na kuuza.
 Diwani wa Kigera Gabriel Ocharo (mwenye suti ya Kijivu) akiwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Musoma Bwire Nyamwero wakiangalia sabuni ya maji iliyotengenezwa na wajasiriamali wakati wa ufunguzi wa moto wa nyika ajira nje nje katika shule ya sekondari ya ufundi ya musoma.
 Diwani wa Kigera Gabriel Ocharo (mwenye suti ya Kijivu) akiwagawia karanga wanafunzi wa Sekondari ya Ufundi Musoma ikiwa ni sehemu ya kutambua kazi za wajasiriamali


Na Thomas Dominick,
Musoma.

MANISPAA ya Musoma Mkoa wa Mara imeahidi kutoa ushirikiano na Club ya Ujasiriamali ya Shule ya Sekondari ya Ufundi Musoma inayofadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) yenye ujumbe wa ajira nje nje kwavijana.

Akizungumza kwenye uzinduzi moto wa nyika wa club hiyo uliofanyika katika viwanja vya shule hiyo Naibu Meya Bwire Nyamwero alisema kuwanjia iliyoonyeshwa na clubu hiyo ni mzuri na inafaa kuungwa mkono na serikali ili kuweza kutatua tatizo la ajira iliyoikumba nchi yetu.

"Kila kukicha utasikia kwenye vyombo vya habari juu ya tatizo la ajira nchini hata nchi za wenzetu huko nje na serikali haiwezi kuwaajira vijana wote wanaomaliza elimu zao lakini kwa hili la kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ni njia sahihi na inapaswa kuungwa mkono,"alisemaNyamwero.

Nyamwero alisema kuwa kwa kuunda vikundi vya ujasiriamali itakuwa nirahisi kuwafikia vijana wengi pamoja na kuwapatia elimu pamoja na kuwawezesha kwa mitaji ya kufanyia biashara zao.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwita Jeremia alisema kuwa mpango huouatafuta dhana ya vijana wasomi kukimbilia maofisini kutafuta kazi ambapo alidai kuwa dhana hiyo ni ya kikoloni kwa kuwa wasomi walipatiwa kazi ya kuajiriwa.

"Tuachane na dhana za kikoloni kinachotakiwa ni kuisaidia serikali
yetu ili kupunguza tatizo la ajira kwa kutumia rasilimali zetu wenyewe katika kujiwezesha na kujikwamua kimaisha ili kuondokana na umasikini,"alisema Mwalimu Jeremia.

Naye Mratibu wa Programu ya Vijana Moto wa Nyika club ya Ujasiriamali ya Sekondari ya ufundi ya Musoma inayofadhiliwa na shirika la kazi Duniani (ILO) Mwl. Magita Nyangole ametoa wito kwa vijana kutumia fursa zilizopo hasa za elimu ya ujasiriamali ili kuwa daraja la kupata ajira.


Mwalimu Nyangole alisema kuwa ameamua kujikita kwa vijana ili waweze kutumia vyanzo vyao na akili walizonazo kwa ajili ya kujishughulisha ili kujikwamua kutoka kwenye umasikini.

"Lengo langu mimi sana ni sisi vijana tujitambue ilikwa pamoja na
kutumia rasilimali tulizonazo akili tulizo nazo ili kuweza kujishughulisha na hii itasaidia kuifanya serikali yetu kupunguza
wimbi la watu ambao kila siku wanailaumu serikali yao,"alisema Mwalimu Magita.

Uzinduzi wa klabu hiyo wenye ujumbe wa ajira nje nje kwa vijana
iliendana na Bonanza la Mpira wa Miguu pamoja na maonyesho ya kazi za wajasiriamali ambao tayari wamepata mafunzo chini ya Mwalimu Magita na wanatengeneza bidhaa za aina mbalimbali kama vile sabuni za miche, maji,bisi, karanga za mayai na bidhaa mbalimbali.
Read More...

CCM MUSOMA MJINI YAJIIMARISHA




 Mkereketwa wa CCM ambaye jina lake halikujulikana mara moja akiwa mbele ya maandamano ya wazee ambao walikuwa wanawasili katika viwanja vya Shule ya Msingi Mukendo kumsikiliza MNEC Vedastus Mathayo Kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama hicho.
  MNEC Vedastus Mathayo Akisalimia na wazee wa CCM Musoma Mjini wakati akiwasili kwenye mkutano hadhara
katika viwanja vya Shule ya Msingi Mukendo
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea katika viwanja vya Shule ya Msingi Mukendo Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mjini na MNEC Taifa Jackson Msome, katikati ni MNEC wa wilaya ya Butiama Christopher Marwa Siagi na kushoto ni MNEC Musoma Mjini Vedastus Mathayo.
 MNEC Musoma Mjini Vedastus Mathayo akiwahutubia mamia ya wananchi wa Musoma katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mukendo.

 *Yafanya mkutano wa Kihistoria
*Chadema yaanza kubomolewa Musoma
*CCM yavuna wanachama 220
*Mamia ya wakazi wafurika viwanja vya Shule ya Msingi Mukendo

Na Thomas Dominick,
Musoma
                                                  
CHAMA cha Mapinduzi  (CCM) Wilaya ya Musoma Mjini Mkoa wa Mara kimevuna  wanachama 220 ambao wamekabidhiwa  kadi mpya na mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa  (NEC) Vedastus Mathayo huku kadi tano za CHADEMA zikirudishwa.

Wanachama hao walipatikana katika mkutano uliofanyika kwenye uwanja maarufu wa Shule ya Msingi Mkendo na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa Wilaya hiyo .

Akihutubia katika Mkutano huo Mathayo alisema kuwa wamejipanga kuimarisha chama hicho kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa ili kujihakikishia inashika dola katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2015.

“Katika kikao chetu kilichofanyika Dodoma chini ya Mwenyekiti wetu Rais Jakaya Kikwete tumejipangia kuboresha huduma za jamii hasa upande wa afya kwani tuna zahanati nyingi sasa tunataka tupate dawa za kutosha pamoja na wataamu wa afya kwa ajili ya wananchi wetu,”alisema Mathayo.

Alisema kuwa CCM baada ya uchaguzi wa ndani ya chama kinajikita zaidi katika kukiimarisha chama hicho na hatimaye kiibuke na ushindi katika chaguzi zijazo za serikali za mitaa ,rais,wabunge na madiwani .

Alisema kuwa kazi ya kubwa kwa sasa iliyo mbele yake ni kushughulikia matatizo  ya wanachama  katika wilaya yake kuhakikisha  ofisi zote za kata wilaya ya musoma zinang’aa na sambamba na kulikomboa jimbo la musoma mjini ambalo lilichukuliwa na chadema.

Alisema kuwa CHADEMA kimeshindwa kutekeleza ahadi walizojitoa katika uchaguzi mkuu na hivyo wakazi wa musoma kujuta kukichagua  cha hicho kilichojaa ahadi hewa lukuki .

“Tulikwisha waambieni wakati tunaomba ridhaa yenu ya kuongoza jimbo kuwa uongozi haujaribiwi sasa majibu mmeshayaona wenyewe tunachowaomba tushirikiane tulirudishe jimbo letu chini ya CCM ili wananchi wafaidi matunda ya chama chao,”alisema.

Alisema kuwa pamoja na kukichagua chama cha demokrasia na maendeleo wakazi wa musoma mjini hakuna kitu chochote  iliyotekelezwa na chama hicho ambapo mbunge wa jimbo la musoma vicent nyerere katika kampeni za kuwania ubunge aliahidi bwawa la kitaji litatoa gesi na badala yake limeendelea kuwa mazalia ya mbu.

Aidha amewaonya wanachama kuachana na makundi ambapo alisema binafsi yeye hataki makundi, hivyo wasahau yaliyopita katika chaguzi  na wagange yajayo
Baada ya hotuba hiyo wanachama 220 walijitokeza na kukabidhiwa kadi mpya za CCM huku  kadi tano za chadema zikirudishwa

Mwisho

Read More...

Friday, November 23, 2012

MNEC MATHAYO ACHANGIA ONGEZEKO LA AJIRA MKOANI MARA






 Mfanyakazi wa Kiwanda cha Mugango Ginnery akichuja mafuta ya kula yanayoitwa LADHA kabla ya kupimwa uzito na kufungwa kwa ajili ya mauzo.
 Gari likiwa tayari kwa ajili ya kupakia marobota ya pamba kwa ajili ya kusafirishwa nje ya mkoa huo.
 Mkurugenzi Joseph Mathayo maarufu Rambo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uzalishaji na utendaji kazi wa kiwanda hicho.
 Wafanyakazi wa kiwanda cha pamba wakitoka nje ya kiwanda baada ya kumaliza uzalishaji huku wakisubiria kuongeza kwa pamba kwa ajili ya kusindikwa.
 Mkurugenzi Joseph Mathayo maarufu Rambo (kushoto) akiwapa maelezo waandishi wa habari waliotembelea kiwandani hapo, kulia ni Augustine Mgendi nyuma ni Shomari Binda.
 Waandishi wa habari na Mkurugenzi wakiwa ndani ya kiwanda cha kusindika mafuta akitoa maelezo jinsi ya ushindikaji wa mafuta.
 Wafanyakazi wakiendelea na uzalishaji wa mafuta ndani ya kiwanda cha Mugango Ginnery kilichopo Wilaya ya Butiama.
 Hii ni nembo inayowakilisha bidhaa yake ya mafuta ambayo yanazalishwa na kiwanda hicho.
Paul Amon akipima uzito mafuta kwenye ndoo ya lita 20 kabla ya kufungwa na kuingizwa sokoni. 

*Ajira kuongezeka mwakani
*huzalisha zaidi ya lita 3000 kwa mpiko mmoja
*wakulima wasema ukombozi umewafikia 

Na Thomas Dominick,

Musoma



KIWANDA cha pamba cha Mugango Ginnery kinachomilikiwa na MNEC Vedastus Mathayo kinatarajiwa kuboreshwa miundombinu yake ili mwakani kitoe ajira nyingi kwa wakazi wa maeneo hayo.



Kiwanda hicho kilichopo katika kata ya Mugango wilaya ya Butiama, Mkoa wa Mara kwa mwaka huu kimetoa ajira za wananchi 175 ambao wanafanya kazi ndani ya kiwanda hicho ambacho kinazalisha mafuta ya kula, marobota ya pamba, pumba na mashudu kwa ajili ya mifugo.



Akizungumza na Waandishi wa habari kiwandani hao, Mkurugenzi Joseph Mathayo maarufu Rambo alisema kuwa wakati wanaanzisha kiwanda hicho walikutana na changamoto nyingi pamoja na kukuta miundombinu ikiwa imeharibiwa kabisa.



“Pamoja na kufanya kazi kubwa ya kuboresha miundombinu ambayo tumetumia pesa nyingi pia tulikutana na wakati mgumu wakati tunafuatilia vibali vya kazi kwa ajili ya kuanza ununuzi wa pamba,”alisema Mathayo.



Alisema kuwa tangu kiwanda hicho mahusiano na jamii inayowazunguka imeboreka zaidi kwa wakazi wa maeneo hayo wamekuwa wakipata misaada mingi ya kibinadamu pamoja na ajira ndani ya kiwanda hicho,”alisema.



Alisema kuwa kiwanda hicho kinazalisha zaidi ya lita 3000 kwa mpiko mmoja ambapokuna matanki mawili na kila tanki la mafuta linachukua lita 150.



Mathayo alitoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Mara na watanzania wanaotembelea mkoa huo kutokuwa na mashska na mafuta hayo kwa kuwa yanapikwa kwa ustadi mkubwa kulinganisha na viwanda vingine ambavyo vinatengeneza mafuta meusi.



“Ninachoweza kusema kuwa watanzania wasjaribu kuyatumia mafuta yetu waone radha yake kwani mafuta yetu ni meupe kuliko mengine kwa kuwa tuna wataalamu wa kutosha ambao wanafanya kazi zao kwa ustadi mkubwa sana,”alisema Mathayo.

Alisema kuwa kwa sasa mafuta hayo yanauzwa katika mikoa mitatu Mkoa wa Simiyu, Mwanza na Mara ambapo pia na bidhaa ya pamba inatoka katika mikoa hiyo hiyo.



Kuhusu suala la kuwasaidia wakulima zana za kilimo kama vile mbegu na mbolea ambapo wanawakopesha kwa kuandikiana na wakati wa manunuzi wanawakata fedha zao za pembejeo na madawa ya pamba.



Mmoja wa mkulima aliyejitambulisha kwa jina la Rajabu Juma mkazi wa Kijiji hicho cha Mugango alisema kuwa wanamshukuru mmiliki wa kiwanda hicho kutokana na mchango wake wa kuinua zao hilo ambalo lilianza kupoteza umaarufu nchini.



“Hatuna cha kumpatia lakini apokee shukurani zetu kwani sasa kilimo cha pamba amekirahisisha sana kwa kuwa tunapata mbegu kwa wakati pamoja na dawa zake hii inatutia moyo sisi wakulima,”alisema Juma.



Kiwanda hicho kilikuwa kinamilikiwa na vyama vya ushirika na kutelekezwa kwa miaka mingi hadi pale MNEC huyo alipoamua kukichukua na kuanza uzalishaji kwa mara ya kwanza mwaka huu.




Read More...

Wednesday, November 21, 2012

MAJAMBAZI YACHINJA YAIBA LAKI 1.76







 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma akiandika kitu fulani kwa ajili ya kuwapatia waandishi wa habari hawapo pichani



Na Thomas  Dominick,
Musoma

MLINZI mmoja wa Kampuni ya ulinzi ya Salama Security  John
Nyaganya(22) ameuawa  kikatili kwa kuchinjwa shingo akiwa lindoni
katika eneo la Mkinyerero,barabara ya majita kata ya Kamunyonge
Manispaa ya Musoma Mkoa wa Mara.

Akizungumza na Habari Moto Moto Mara Ofisini kwake Jana  kamanda wa jeshi
la polisi mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma alisema kuwa tukio hilo
limetokea  Alfajiri ya tarehe 21 mwaka huu.

Mwakyoma alisema  kuwa  alfajili hiyo mwili wa marehemu mlinzi wa
kampuni ya Samala security uligunduliwa  ukiwa umekatwa  shingo wakati
akiwa mwenye lindo la   la Pub ijulikanayo kwa jina la Pub ya Tulivu
mali ya mfanyabiashara mmoja  Paulo Karege(34) mkazi wa barabara ya
majita .

 Kamanda alisema kuwa  marehemu alikuwa ameajiliwa  na kampuni ya
Salama security  kulinda pub hiyo na uchunguzi  umeonesha kuwa  wauaji
hao walimuua kwa kutumia kitu chenye ncha kali na kasha  kuiba sanduku
 mbili za bia na viti vya plasitiki saba zenye thamani ya shilingi za
kitanzania 176,000/=.

 Alisema kuwa  ufatuliaji wa kina unafanyika  katika maeneo mbalimbali
ya   mji na nje ya mji ili kubaini waharifu hao  na kuwakamata ili
hatua za kisheria  zichukuliwe  haraka iwezekanayo.

Kamanda huyo aliongeza kuwa  mpaka sasa amekamatwa mtu mmoja (jina
limehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi) akiwa na nondo tatu,mtarimbo
,pinde na mishale mitatu,kirungu na nguo za kike.

Alisema wahalifu hao walikuwa wamevaa nguo za kike maarufu hijabu
(camouflage) ili kuficha sura ao wakati walipokuwa wakifanya kitendo
hicho na ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa  mara wanapoona watu
wanaowatilia mashaka pia amewataka kuimalisha vikundi vya ulinzi
shirikishi ili  kupunguza uharifu kwa wahalifu wengi wamo miongoni mwa
wananchi.


Mwisho.
Read More...