Gari likiwa tayari kwa ajili ya kupakia marobota ya pamba kwa ajili ya kusafirishwa nje ya mkoa huo.
Mkurugenzi Joseph Mathayo maarufu Rambo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uzalishaji na utendaji kazi wa kiwanda hicho.
Wafanyakazi wa kiwanda cha pamba wakitoka nje ya kiwanda baada ya kumaliza uzalishaji huku wakisubiria kuongeza kwa pamba kwa ajili ya kusindikwa.
Mkurugenzi Joseph Mathayo maarufu Rambo (kushoto) akiwapa maelezo waandishi wa habari waliotembelea kiwandani hapo, kulia ni Augustine Mgendi nyuma ni Shomari Binda.
Waandishi wa habari na Mkurugenzi wakiwa ndani ya kiwanda cha kusindika mafuta akitoa maelezo jinsi ya ushindikaji wa mafuta.
Wafanyakazi wakiendelea na uzalishaji wa mafuta ndani ya kiwanda cha Mugango Ginnery kilichopo Wilaya ya Butiama.
Hii ni nembo inayowakilisha bidhaa yake ya mafuta ambayo yanazalishwa na kiwanda hicho.
Paul Amon akipima uzito mafuta kwenye ndoo ya lita 20 kabla ya kufungwa na kuingizwa sokoni.
*Ajira kuongezeka mwakani
*huzalisha zaidi ya lita 3000 kwa mpiko mmoja
*wakulima wasema ukombozi umewafikia
Na Thomas Dominick,
Musoma
KIWANDA cha pamba cha Mugango
Ginnery kinachomilikiwa na MNEC Vedastus Mathayo kinatarajiwa kuboreshwa miundombinu
yake ili mwakani kitoe ajira nyingi kwa wakazi wa maeneo hayo.
Kiwanda hicho kilichopo
katika kata ya Mugango wilaya ya Butiama, Mkoa wa Mara kwa mwaka huu kimetoa
ajira za wananchi 175 ambao wanafanya kazi ndani ya kiwanda hicho ambacho
kinazalisha mafuta ya kula, marobota ya pamba, pumba na mashudu kwa ajili ya
mifugo.
Akizungumza na Waandishi wa
habari kiwandani hao, Mkurugenzi Joseph Mathayo maarufu Rambo alisema kuwa
wakati wanaanzisha kiwanda hicho walikutana na changamoto nyingi pamoja na
kukuta miundombinu ikiwa imeharibiwa kabisa.
“Pamoja na kufanya kazi kubwa
ya kuboresha miundombinu ambayo tumetumia pesa nyingi pia tulikutana na wakati
mgumu wakati tunafuatilia vibali vya kazi kwa ajili ya kuanza ununuzi wa pamba,”alisema
Mathayo.
Alisema kuwa tangu kiwanda
hicho mahusiano na jamii inayowazunguka imeboreka zaidi kwa wakazi wa maeneo
hayo wamekuwa wakipata misaada mingi ya kibinadamu pamoja na ajira ndani ya
kiwanda hicho,”alisema.
Alisema kuwa kiwanda hicho
kinazalisha zaidi ya lita 3000 kwa mpiko mmoja ambapokuna matanki mawili na kila
tanki la mafuta linachukua lita 150.
Mathayo alitoa wito kwa
wananchi wa Mkoa wa Mara na watanzania wanaotembelea mkoa huo kutokuwa na
mashska na mafuta hayo kwa kuwa yanapikwa kwa ustadi mkubwa kulinganisha na
viwanda vingine ambavyo vinatengeneza mafuta meusi.
“Ninachoweza kusema kuwa
watanzania wasjaribu kuyatumia mafuta yetu waone radha yake kwani mafuta yetu
ni meupe kuliko mengine kwa kuwa tuna wataalamu wa kutosha ambao wanafanya kazi
zao kwa ustadi mkubwa sana,”alisema Mathayo.
Alisema kuwa kwa sasa mafuta
hayo yanauzwa katika mikoa mitatu Mkoa wa Simiyu, Mwanza na Mara ambapo pia na
bidhaa ya pamba inatoka katika mikoa hiyo hiyo.
Kuhusu suala la kuwasaidia
wakulima zana za kilimo kama vile mbegu na mbolea ambapo wanawakopesha kwa
kuandikiana na wakati wa manunuzi wanawakata fedha zao za pembejeo na madawa ya
pamba.
Mmoja wa mkulima aliyejitambulisha
kwa jina la Rajabu Juma mkazi wa Kijiji hicho cha Mugango alisema kuwa
wanamshukuru mmiliki wa kiwanda hicho kutokana na mchango wake wa kuinua zao
hilo ambalo lilianza kupoteza umaarufu nchini.
“Hatuna cha kumpatia lakini
apokee shukurani zetu kwani sasa kilimo cha pamba amekirahisisha sana kwa kuwa
tunapata mbegu kwa wakati pamoja na dawa zake hii inatutia moyo sisi wakulima,”alisema
Juma.
Kiwanda hicho kilikuwa
kinamilikiwa na vyama vya ushirika na kutelekezwa kwa miaka mingi hadi pale
MNEC huyo alipoamua kukichukua na kuanza uzalishaji kwa mara ya kwanza mwaka
huu.
0 comments:
Post a Comment