MNEC Vedastus Mathayo Akisalimia na wazee wa CCM Musoma Mjini wakati akiwasili kwenye mkutano hadhara
katika viwanja vya Shule ya Msingi Mukendo
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea katika viwanja vya Shule ya Msingi Mukendo Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mjini na MNEC Taifa Jackson Msome, katikati ni MNEC wa wilaya ya Butiama Christopher Marwa Siagi na kushoto ni MNEC Musoma Mjini Vedastus Mathayo.
MNEC Musoma Mjini Vedastus Mathayo akiwahutubia mamia ya wananchi wa Musoma katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mukendo.
*Yafanya mkutano wa Kihistoria
*Chadema yaanza kubomolewa Musoma
*CCM yavuna wanachama 220
*Mamia ya wakazi wafurika viwanja vya Shule ya Msingi Mukendo
Na Thomas Dominick,
Musoma
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Musoma Mjini Mkoa wa Mara
kimevuna wanachama 220 ambao
wamekabidhiwa kadi mpya na mjumbe wa Halmashauri
Kuu Taifa (NEC) Vedastus Mathayo huku
kadi tano za CHADEMA zikirudishwa.
Wanachama hao walipatikana katika
mkutano uliofanyika kwenye uwanja maarufu wa Shule ya Msingi Mkendo na
kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa Wilaya hiyo .
Akihutubia katika Mkutano huo
Mathayo alisema kuwa wamejipanga kuimarisha chama hicho kuanzia ngazi ya shina
hadi Taifa ili kujihakikishia inashika dola katika uchaguzi mkuu utakaofanyika
mwaka 2015.
“Katika kikao chetu
kilichofanyika Dodoma chini ya Mwenyekiti wetu Rais Jakaya Kikwete tumejipangia
kuboresha huduma za jamii hasa upande wa afya kwani tuna zahanati nyingi sasa
tunataka tupate dawa za kutosha pamoja na wataamu wa afya kwa ajili ya wananchi
wetu,”alisema Mathayo.
Alisema kuwa CCM baada ya
uchaguzi wa ndani ya chama kinajikita zaidi katika kukiimarisha chama hicho na
hatimaye kiibuke na ushindi katika chaguzi zijazo za serikali za mitaa
,rais,wabunge na madiwani .
Alisema kuwa kazi ya kubwa
kwa sasa iliyo mbele yake ni kushughulikia matatizo ya wanachama
katika wilaya yake kuhakikisha
ofisi zote za kata wilaya ya musoma zinang’aa na sambamba na kulikomboa
jimbo la musoma mjini ambalo lilichukuliwa na chadema.
Alisema kuwa CHADEMA kimeshindwa
kutekeleza ahadi walizojitoa katika uchaguzi mkuu na hivyo wakazi wa musoma
kujuta kukichagua cha hicho kilichojaa
ahadi hewa lukuki .
“Tulikwisha waambieni wakati
tunaomba ridhaa yenu ya kuongoza jimbo kuwa uongozi haujaribiwi sasa majibu
mmeshayaona wenyewe tunachowaomba tushirikiane tulirudishe jimbo letu chini ya
CCM ili wananchi wafaidi matunda ya chama chao,”alisema.
Alisema kuwa pamoja na kukichagua
chama cha demokrasia na maendeleo wakazi wa musoma mjini hakuna kitu chochote iliyotekelezwa na chama hicho ambapo mbunge wa
jimbo la musoma vicent nyerere katika kampeni za kuwania ubunge aliahidi bwawa
la kitaji litatoa gesi na badala yake limeendelea kuwa mazalia ya mbu.
Aidha amewaonya wanachama
kuachana na makundi ambapo alisema binafsi yeye hataki makundi, hivyo wasahau
yaliyopita katika chaguzi na wagange
yajayo
Baada ya hotuba hiyo
wanachama 220 walijitokeza na kukabidhiwa kadi mpya za CCM huku kadi tano za chadema zikirudishwa .
Mwisho
0 comments:
Post a Comment