Sunday, November 18, 2012

WASICHANA 4000 KUKEKETWA TARIME MARA



                                           Picha ya Mtoto wa Kike akikeketwa




*Ni kuanzia Novemba hadi Disemba mwaka huu
*Shirika la CDF kutoa elimu ili vitendo hivyo vikomeshwe
*Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya watu Duniani (UNFPA) laiomba Serikali kutunga  sheria ya kukomesha vitendo hivyo
                               

Na Thomas Dominick,
Musoma.

ZAIDI ya wasichana wapatao 4000 wanatarajia kufanyiwa ukeketaji mwezi
Disemba mwaka huu katika baadhi ya koo Wilayani  Tarime Mkoa wa Mara.

Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu wa shirika lisilo la
kiserikali la Children Dignity Forum(CDF) Joram Wimmo alisema kuwa baadhi ya koo katika wilaya hiyo zinajiandaa kufanya ukeketaji wa wasichana mwezi ujao .

Alisema kuwa  Shirika hilo la FDC limefanya utafiti mdogo unaoonyesha
 kuwa zaidi ya wasichana na watoto wa kike 4000 wanatarajiwa kukeketwa kati ya miezi hii miwili.

Wimmo alisema  jitihada za makusudi zinahitajika hasa katika utoaji wa
  elimu ili kuhakikisha vitendo vya ukeketaji wa wasichana Mkoani Mara unakomeshwa  ili kunusuru madhara makubwa ya kiafya na ukatili unaokwamisha shughuli za maendeleo ya kiuchumi.

“Msimu wa ukeketaji wa wasichana umewadia huwa ni kati ya  mwezi huu
na mwezi ujao kwa kuwa ndio miezi ambayo watoto wengi wa kike wanakuwa katika kipindi cha likizo”alisema Wimmo.

Alifafanua kuwa sio kila mwaka ukeketaji huo unafanyika bali

hufanyika mara mbili kwa mwaka unaogawanyika mara mbili kama huu wa 2012 na kwamba shirika hilo la CDF mkoani Mara limeanza kuchukua hatua.

Alisema  atashirikiana mashirika mbalimbali  hasa kituo cha Masanga
kilichopo Wilayani  Tarime ambacho ndio kimbilio la wasichana wasiotaka kufanyiwa ukeketaji na kuondoa hofu miongoni mwa wasichan hao kwa msimu huu.

Pia atashirikiana na viongozi wa Serikali ya kijiji kwa kutoa elimu
mbadala ili waweze kupata njia mbadala  na kuwapa elimu ya kisimamaia haki zao za msingi  kwa kujua athari za ukeketaji ili kuepukana nao.

Licha ya shirika hilo kufanya utafiti pia kuna shirika la Kimataifa la

maendeleo ya watu Duniani (UNFPA) limefanya utafiti Wilayani humo na kubaini  kuwepo kwa idadi ya wasichana hao kufanyiwa ukeketaji na wameiomba Serikali itunge sheria  ya kukomesha vitendo hivyo kutoa Wizara husika.

MWISHO

0 comments:

Post a Comment