Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma akiandika kitu fulani kwa ajili ya kuwapatia waandishi wa habari hawapo pichani
Na Thomas Dominick,
Musoma
MLINZI mmoja wa Kampuni ya
ulinzi ya Salama Security John
Nyaganya(22) ameuawa kikatili kwa kuchinjwa shingo akiwa lindoni
katika eneo la
Mkinyerero,barabara ya majita kata ya Kamunyonge
Manispaa ya Musoma Mkoa wa
Mara.
Akizungumza na Habari Moto
Moto Mara Ofisini kwake Jana kamanda wa
jeshi
la polisi mkoa wa Mara
Absalom Mwakyoma alisema kuwa tukio hilo
limetokea Alfajiri ya tarehe 21 mwaka huu.
Mwakyoma alisema kuwa
alfajili hiyo mwili wa marehemu mlinzi wa
kampuni ya Samala security
uligunduliwa ukiwa umekatwa shingo wakati
akiwa mwenye lindo la la Pub ijulikanayo kwa jina la Pub ya Tulivu
mali ya mfanyabiashara
mmoja Paulo Karege(34) mkazi wa barabara
ya
majita .
Kamanda alisema kuwa marehemu alikuwa ameajiliwa na kampuni ya
Salama security kulinda pub hiyo na uchunguzi umeonesha kuwa wauaji
hao walimuua kwa kutumia kitu
chenye ncha kali na kasha kuiba sanduku
mbili za bia na viti vya plasitiki saba zenye
thamani ya shilingi za
kitanzania 176,000/=.
Alisema kuwa
ufatuliaji wa kina unafanyika
katika maeneo mbalimbali
ya mji na nje ya mji ili kubaini waharifu
hao na kuwakamata ili
hatua za kisheria zichukuliwe
haraka iwezekanayo.
Kamanda huyo aliongeza
kuwa mpaka sasa amekamatwa mtu mmoja
(jina
limehifadhiwa kwa ajili ya
uchunguzi) akiwa na nondo tatu,mtarimbo
,pinde na mishale
mitatu,kirungu na nguo za kike.
Alisema wahalifu hao walikuwa
wamevaa nguo za kike maarufu hijabu
(camouflage) ili kuficha sura
ao wakati walipokuwa wakifanya kitendo
hicho na ametoa wito kwa
wananchi kutoa taarifa mara wanapoona
watu
wanaowatilia mashaka pia
amewataka kuimalisha vikundi vya ulinzi
shirikishi ili kupunguza uharifu kwa wahalifu wengi wamo
miongoni mwa
wananchi.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment