Na Thomas Dominick,
Tarime.
MKUU wa Mkoa wa Mara John Tuppa
ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Tarime kufyeka mazao yote yaliyomo
ndani ya eneo la Serikali ili kuondo migogoro ya aridhi ya wananchi wa
kijiji cha Ng’ereng’ere na kijiji cha Kurutamba.
Agizo hilo
limetolewa jana, wakati alipokuwa katika ziara ya kukagua
eneo hilo la Serikali wilayani humo ambalo ndilo linalosababisha
machafuko ya mara kwa mara ya wananchi wa vijiji hivyo viwili.
Tuppa
alisema kuwa mazao hayo yaliyomo ndani ya shamba hilo yamekuwa
yakisababisha vijiji hivyo kupigana hasa baada ya kila mwananchi
kutakiwa kuwa katika kijiji chake kwa kuwa wananchi hao wamekuwa
wakilima shamba hilo kinyume cha sheria.
Pia
ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya wilaya hiyo kuhakikisha wale wote
wanaochochea mapigano kuanzia madiwani ,wazee wa kimila pamoja na wale
wote waliohusika katika mauaji ya mwananchi mmoja hivi karibuni.
Aliwaagiza
watendaji wa vijiji vyote viwili kuhakikisha wanawajibika ipasavyo
ili kuepusha migogoro ya ardhi katika eneo hilo kwa kuonesha mipaka
halali ambayo itasaidia kila mmoja kuwajibika kulingana na ramani ya
mipaka itakayokuwa imeoneshwa.
“Viongozi wa kitongoji na
kata zote ni kwamba wafuate utaratibu tuliopeana tunaomba ufanyike kwani
kama ungekuwa umefanyika sisi tusingekuja hapa matatizo hayo tote
mngekuwa mmesha yatatua na sio kusubiri mpaka madhara yatokee
tumechoshwa na migogoro ya Tarime ya mara kwa mara”Alisema Tuppa.
Alisema
kuwa kitu kikubwa hasa kinachowachanganya wananchi ni mipaka ya kijiji
na mipaka ya eneo lililopo ambalo ndilo linaloleta matatizo hivyo
ambaye hata ridhika afate utaratibu na sio kuchua sheria mikononi.
Kwa
Upande wa wahanga wa mapigano hayo wakazi wa kijiji cha Nyamaraga
walisema kuwa wao wanachotaka ni Serikali kuingilia kati kwa kuwasaidia
kutatua matatizo hayo kwani hata wao wamechoshwa na mapigano ya mara
kwa mara na wanachokitaka sasa ni maendeleo.
Pia wameiomba
serikali kuwekeza kitu chochote katika eneo hilo ambalo ndio chanzo cha
migogoro ya mara kwa mara kwa kuwa ni eneo kubwa sana lenye hekta 193.3
na ambalo lipo wazi na lenye rutuba hivyo kufanya wananchi kulima eneo
hilo kinyume cha sheria au wapewe sehemu nyingine ili wapate sehemu ya
kulima mazao ya chakula.
“Sababu hasa inayosababisha mapigano
kati ya vijiji hivi viwili ni oparesheni ya vijiji ambayo inambidi kila
mtu kuwa katika kijiji chake hii ndio iliyosababisha matabaka ya kila
koo kujitenga sasa mazao waliyokuwa wanalina katika shamba hilo nani
atayasimamia na ndio yanayoleta migogoro”alisema Christopher Mlimi.
Waliongeza
kuwa toka mwaka 1992 eneo hilo ndilo limekuwa chachu ya mapigano baina
ya koo mbalimbali katika wilaya hiyo hivyo serikali ichukue hatua za
haraka ili kunusuru vifo vanavyotokana na shamba hilo.
Mwisho.
Sunday, November 18, 2012
RC AAGIZA MAZAO YAFYEKWE ILI KUNUSURU MIGOGORO TARIME *asema mipaka ionyeshwe vizuri *wananchi wataka Serikali kuwekeza eneo hilo
by Unknown
0 comments:
Post a Comment