Monday, November 19, 2012

MOTO WA AJIRA WAWASHWA MKOANI MARA

WANAFUNZI WA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI WAKIONYESHA BIDHAA ZAO WALIZOZITENGENEZA BAADA YA KUPATA MAFUNZO YA UTENGENEZAJI SABUNI 

 WANAFUNZI WA UFUNDI SEREMALI WA MPANGO WA UWIANO KATI YA ELIMU YA WATU WAZIMA NA JAMII (MUKAJA)

 MWL. MAGITA NYANGOLE MWENYE SHATI JEUPE AKIWAELEKEZA WANAFUNZI WA UJASIRIAMALI KUTOKA KULIA NI TADEO RAPHAEL, DAUD RAYMOND, JUMA DICKSON, ANTONY RAPHAEL HAMIS JAMES. 


 WANAFUNZI WA UJASIRIAMALI WAKIPATA MAELEKEZO TOKA KWA MWL. MAGITA NYANGOLE KUTOKA KULIA NI MICHAEL ALOYCE, DINA KERARYO, ZEBIDA MKANGARA.

*ILO yajitosa kuwaokoa vijana Mkoani Mara
*Mfumo wa elimu wamsukuma mwl. Nyangole kuwainua vijana
Na Thomas Dominick,
Musoma

MOTO wa Fursa za ajira kwa vijana umewashwa katika Manispaa ya Musoma Mkoani Mara baada ya vijana kupata elimu ya Ujasiriamali unaoendeshwa chini ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoani hapa ina
yoratibiwa na club ya Ujasiriamali ya Sekondari ya ufundi ya Musoma inayofadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO).

Wakizungumza na Habari Moto Moto Mara baadhi ya wanafunzi walisema kuwa mafunzo hayo yanawasaidia kuepukana na utegemezi kutoka kwa wazazi wao na kuweza kujipatia ajira ya kujiajiri wenyewe na kuinua pato katika familia na kuinua uchumi wa Taifa.

Mwanafunzi aliyejitambulishakwa jina la Eva Kasimbi amesema kuwa mpango huo unatoa ajira kwa vijana na kuacha kukaa kwenye vijiwe ambavyo hazina tija kwao na amesema kuwa mafunzo ambayo wameshayapata ni pamoja na utengenezaji wa sabuni za aina mbalimbali.

Mshiriki mwingine Michael Kate ameiomba Serikali iwasaidie
wajasiriamali kupata mikopo hasa vijana ili kuweza kujikwamua kimaisha pamoja na kuisaidia SIDO kuweza kuwapatia fedha za kutosha ili kuendesha mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali.

Naye Mratibu wa Programu ya Vijana Moto wa Nyika inayoratibiwa na club ya Ujasiriamali ya Sekondari ya ufundi ya Musoma inayofadhiliwa na shirika la kazi Duniani (ILO) Mwl. Magita Nyangole ametoa wito kwa vijana kutumia fursa zilizopo hasa za elimu ya ujasiriamali ili kuwa daraja la kupata ajira.

Mwl. Nyangole amesema kuwa amesukumwa na tatizo la elimu yetu nchini kutotoa elimu kwa vijana ya kujiajiri badala yake inafundisha jinsi vijana watakapomaliza shule kutafuta ajira serikalini au kwenya mashirika makubwa hivyo vijana kufumbua macho nakuwa na utashi wa kuwabadilisha vijana ili kuona fursa zilizopo na kuzitumia ipasavyo.

Ameiomba viongozi wa Serikali kuwasaidia na kuwaunganisha vijana vijana ili waweze kufaidika na fursa zilizopo ambapo amesema kuwa endapo vijana zaidi ya 1000 wakipata mafunzo ya ujasiriamali yatawanufaisha wao na jamii inayowazunguka pamoja na kuwapatia ajira vijana wenzao.

Mpango huo wa Oparesheni Moto wa Nyika au Kazi Nje Nje unategemea kuzinduliwa rasmi Novemba 23 mwaka huu katika viwanja vya shule ya msingi Mukendo.

Pia amewaomba wakazi wa MKoa wa Mara kwa ujumla wajitokeze ili waweze kupata elimu na kujua kazi zinazofanywa na vikundi mbalimbali ambavyo tayari vimeundwa.

Kikundi cha uigizaji kinachoitwa Musoma Enveroment Consavation Awereness Group (MECAG), Mpango wa Uwiano kati ya elimu ya watu wazima na jamii (MUKAJA) na wajasiriamali waliopo SIDO.

MWISHO

0 comments:

Post a Comment