Monday, November 26, 2012

UZINDUZI WA MOTO WA NYIKA WAFUNIKA MKOANI MARA

 Naibu Meya Bwire Nyamwero akionyeshwa moja ya mabanda ya kuhifadhia kuku lililotengenezwa na Vijana wajasiriamali wa Shule ya Ufundi ya Musoma Mkoani Mara 
 Naibu Meya Bwire Nyamwero akizungumza jambo na wajasiriamali walioleta bidhaa zao kwa ajili ya maonyesho na kuuza.
 Diwani wa Kigera Gabriel Ocharo (mwenye suti ya Kijivu) akiwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Musoma Bwire Nyamwero wakiangalia sabuni ya maji iliyotengenezwa na wajasiriamali wakati wa ufunguzi wa moto wa nyika ajira nje nje katika shule ya sekondari ya ufundi ya musoma.
 Diwani wa Kigera Gabriel Ocharo (mwenye suti ya Kijivu) akiwagawia karanga wanafunzi wa Sekondari ya Ufundi Musoma ikiwa ni sehemu ya kutambua kazi za wajasiriamali


Na Thomas Dominick,
Musoma.

MANISPAA ya Musoma Mkoa wa Mara imeahidi kutoa ushirikiano na Club ya Ujasiriamali ya Shule ya Sekondari ya Ufundi Musoma inayofadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) yenye ujumbe wa ajira nje nje kwavijana.

Akizungumza kwenye uzinduzi moto wa nyika wa club hiyo uliofanyika katika viwanja vya shule hiyo Naibu Meya Bwire Nyamwero alisema kuwanjia iliyoonyeshwa na clubu hiyo ni mzuri na inafaa kuungwa mkono na serikali ili kuweza kutatua tatizo la ajira iliyoikumba nchi yetu.

"Kila kukicha utasikia kwenye vyombo vya habari juu ya tatizo la ajira nchini hata nchi za wenzetu huko nje na serikali haiwezi kuwaajira vijana wote wanaomaliza elimu zao lakini kwa hili la kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ni njia sahihi na inapaswa kuungwa mkono,"alisemaNyamwero.

Nyamwero alisema kuwa kwa kuunda vikundi vya ujasiriamali itakuwa nirahisi kuwafikia vijana wengi pamoja na kuwapatia elimu pamoja na kuwawezesha kwa mitaji ya kufanyia biashara zao.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwita Jeremia alisema kuwa mpango huouatafuta dhana ya vijana wasomi kukimbilia maofisini kutafuta kazi ambapo alidai kuwa dhana hiyo ni ya kikoloni kwa kuwa wasomi walipatiwa kazi ya kuajiriwa.

"Tuachane na dhana za kikoloni kinachotakiwa ni kuisaidia serikali
yetu ili kupunguza tatizo la ajira kwa kutumia rasilimali zetu wenyewe katika kujiwezesha na kujikwamua kimaisha ili kuondokana na umasikini,"alisema Mwalimu Jeremia.

Naye Mratibu wa Programu ya Vijana Moto wa Nyika club ya Ujasiriamali ya Sekondari ya ufundi ya Musoma inayofadhiliwa na shirika la kazi Duniani (ILO) Mwl. Magita Nyangole ametoa wito kwa vijana kutumia fursa zilizopo hasa za elimu ya ujasiriamali ili kuwa daraja la kupata ajira.


Mwalimu Nyangole alisema kuwa ameamua kujikita kwa vijana ili waweze kutumia vyanzo vyao na akili walizonazo kwa ajili ya kujishughulisha ili kujikwamua kutoka kwenye umasikini.

"Lengo langu mimi sana ni sisi vijana tujitambue ilikwa pamoja na
kutumia rasilimali tulizonazo akili tulizo nazo ili kuweza kujishughulisha na hii itasaidia kuifanya serikali yetu kupunguza
wimbi la watu ambao kila siku wanailaumu serikali yao,"alisema Mwalimu Magita.

Uzinduzi wa klabu hiyo wenye ujumbe wa ajira nje nje kwa vijana
iliendana na Bonanza la Mpira wa Miguu pamoja na maonyesho ya kazi za wajasiriamali ambao tayari wamepata mafunzo chini ya Mwalimu Magita na wanatengeneza bidhaa za aina mbalimbali kama vile sabuni za miche, maji,bisi, karanga za mayai na bidhaa mbalimbali.

0 comments:

Post a Comment