Na Thomas Dominick,
Musoma
MKAZI mmoja wa kijiji cha Nyiberekere
kilichopo Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara Nyabuke Maheri ,ameuawa kwa
kupigwa mawe kisha kuchomwa moto kwa tuhuma za uchawi.
Kwa mujibu wa
Taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Absalom Mwakyoma,Bibi huyo
mwenye umri wa miaka 68 alifikwa na mauti Februari 2 majira ya saa 10 jioni
baada ya watu kadhaa kufika nyumbani kwake na kuubwaga mwili wa mtu
aliyedaiwa kuuawa kichawi na bibi huyo Februari 1.
Watu hao
wanaoelezwa kuwa wa ukoo mmoja na bibi huyo waliamua kujichukulia sheria
mkononi baada ya marehemu Nyabunke kuwajibu kuwa hata wakimsusia maiti hiyo
hawana uwezo wa kumfanya lolote.
Kamanda Mwakyoma alifafanua kuwa,hata
hivyo mwili wa marehemu Kitene Kasinde(50)ulizikwa jana (feb 3)baada ya
viongozi wa eneo hilo na jeshi la polisi kushauriana na ndugu hao kuondoa
tofauti zao kwa kutoamani dhana ya uchawi na badala yake washirikiane kuusiri
mwili huo.
Akizungumzia tabia ya wananchi kujichukulia sheria mkonono
Mwakyoma ameapa kuwashughulikia ipasavyo wale wote wanaoendeleza tabia
hiyo na kutoa wito kwa wanancho kushirikiana na kutoa taarifa kwa polisi
pindi waonapo matukio ya aina hiyo.
MWISHO
Monday, February 4, 2013
IMANI ZA KISHIRIKINA ZAMTOA UHAI
by Unknown
0 comments:
Post a Comment