Gari aina ya Ardeo D 4 Toyota lenye namba ya usajili T 904 BET ikiwa chini ya daraja lililopo njia ya kuelekea Majita Road baada ya dereva wa gari hilo Himis Mchongole kushindwa kulithibiti na kuingia Darajani karibu na makazi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Askari wa Usalama Barabarani akiwa katika shughuli ya kupima eneo la ajali ya gari lenye namba T 904 BET lililopata ajali Leo asubuhi
Kijana Hamis Mchongole ambaye alikuwa anaendesha gari lililopata ajali akiwa katika gari la Polisi baada ya kuokolewa kutoka ndani ya gari hiyo.
Askari wa Usalama barabarani akiendelea na upimaji wa ajali hiyo.
Na Thomas Dominick,
Musoma
Gari lenye namba T 904 BET lililokuwa likiendeshwa na kijana Hamis Mchongole lilianguka na kuharibika vibaya baada ya dereva huyo kushindwa kulimudu na kuingia darajani katika barabara ya Majita, Manispaa ya Musoma, Mkoa wa Mara.
Tukio hilo limetokea Leo asubuhi katika daraja linalotenganisha kati ya mtaa wa mukendo na Mwisenge maarufu Majita Road, inadaiwa kuwa dereva wa aliyekuwa anaendesha gari hilo ni mwosha magari wa eneo la Uwanja wa Ndege Mjini hapo.
Mwandishi wa Blog hii alifika katika eneo la tukio na kudodosa kisa cha gari hiyo kuingia darajani humo ambapo baadhi ya mashuhuda walisema kuwa kijana huyo alikuwa anaendesha gari hilo kwa mwendo wa kasi.
Inadaiwa kuwa gari hiyo ilipeleka kwa mwosha magari kwa ajili ya ya kufanyiwa usafi lakini aliacha funguo za gari, jina la Mmiliki wa gari hilo halikuweza kupatikana mara moja ili kuelezea ni jinsi gani gari lake liliendeshwa na mwosha magari huyo na kama alikuwa amemuagiza.
MWISHO
Wednesday, February 13, 2013
MWOSHA MAGARI AANGUSHA GARI LA MTEJA WAKE
by Unknown
0 comments:
Post a Comment