Baadhi ya Waandishi wa habari wa Mkoa wa Mara wakiwa katika chumba cha mchungaji Daudi Makoye kwa ajili ya kwenda kusikilza wito walioitiwa na mchungaji huyo.
MWENYEKITI wa Kanisa la Waadventista
wasabato Jimbo la Mara na Ukerewe (Mara Conference), Daudi Makoye amekanusha
vikali mbele ya waandishi wa habari taarifa iliyotolewa na Radio Free Africa kuwa Mchungaji wa Kanisa hilo la Ukerewe, Emmanuel Tarara kuwa amebaka mtoto mwenye
umri wa miaka minane na kwamba huyo si mchungaji wa kanisa hilo.
Na Thomas Dominick,
Musoma.
Musoma.
MWENYEKITI wa Kanisa la Waadventista
wasabato Jimbo la Mara na Ukerewe (Mara Conference), Daudi Makoye amekanusha
vikali taarifa iliyotolewa na Radio Free Africa kuwa Mchungaji wa Kanisa la
Waadvetista wa Sabato la Ukerewe, Emmanuel Tarara kuwa amebaka mtoto mwenye
umri wa miaka minane na kwamba huyo si mchungaji wa kanisa hilo.
Sambamba na kumtaka mtangazaji wa
redio hiyo Jovinta Kaijage kukanusha mara moja na kuomba radhi kwa kanisa hilo
na watanzania kwa ujumla la sivyo watamchukulia hatua yeye na chombo chake.
Akizungumza na waandishi wa habari
katika Kanisa la waadventisa wa sabato la Kamunyonge, Mchungaji Makoye alisema kuwa taarifa hiyo iliyotangazwa juzi katika
kipindi chake cha “Matukio” kinachotangazwa kuanzia saa moja ya asubuhi, ilitangazwa
na mwandishi wake Jovinta Kaijage kutoka Ukerewe.
"Tunapenda kukanusha vikali
taarifa hii kwa sababu hauna ukweli wowote Kanisa la Waadventista Wasabato kwa
sasa ina wachungaji watatu katika wilaya ya Ukerewe.”alisema Mchungaji Makoye.
Aliwataja wachungaji wa Ukerewe ni
pamoja na Mchungaji Elifamili Kashanga anayesimamia mtaa wa Mrutunguru,
Mchungaji Kapete Mafuru anayesimamia mtaa wa Ilangara.
Mitaa mingine inasimamiwa na Mchungaji
Zefa Ayugi anayesimamia mtaa wa Buhima na mtaa wa Nansio unasimamiwa na Mzee wa
kanisa ndugu Staford Maiga anayekaimu nafasi ya mchungaji Daniel Muhono
aliyehamia Mtaa wa Buturi hadi atakapopelekwa mchungaji mwingine.
Alisema kuwa kutokana na taarifa
hizo waliwasiliana na Mzee wa kanisa, Staford Maiga wa Nansio ambaye
walizungumza nae kwa simu juu ya jina hilo na kuthibitisha kuwa Emmanuel
Tarara hata si mshiriki wa kanisa hilo.
Aidha amewaomba waandishi wa
habari na hasa wa chombo kilihusika (RFA) kutoa taarifa sahihi iliyofanyiwa uchunguzi
na kuhakikishwa kisha kuutangaza kwa wananchi.
“Waandishi wa habari ni watu
waliiopewa dhamana ya kuelemisha na kudumisha amani ya umma ya watanzania
na kokote na kwamba ni taarifa za uhakika tua nizo zinazosikika,
hivyo si vizuri kutoa taarifa isiyo sahihi na yenye malengo mbaya
kwa hisia za watu na inayoweza kuleta mfarakano na fitina katika
jamii,”alisema.
Pia taarifa isitolewe ambayo inaweza
kuleta picha mbaya au kupaka matope dhehebu na kuharibia sifa ya kanisa hivyo pamoja
amemtaka Mwandishi huyo aombe radhi kwa jumuia ya kanisa la Waadventista
Wasabato na watanzania wengine waliosikiliza habari hiyo kurekebisha
taarifa hiyo haraka.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment