*Mwisho baada ya kuona imeshindikana wakatoboa siri
* wasema mtego huo ulikuwa haumuachi madarakani
*Mwenyekiti wa Chadema Mkoa ajikanyanga kwenye maelezo yake
Diwani wa Kigera (CUF) Gabriel Ocharo akimbana Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kwa madai ya ukiukwaji kwa taratibu za kuwasilisha Bajeti ya Manispa ya Musoma ya Mwaka 2013/14, Bajeti hiyo iliwasilishwa Wizara ya Fedha bila kukaa kwa kamati za Manispaa hiyo kisha kupitishwa kwenye Kikao cha Madiwani.
Angela Derrick Diwani wa Kata ya kamnyonge (CHADEMA) akieleza masikitiko yake yaliyofanywa na watendaji wa Manispaa ya Musoma kwa ukiukwaji kwa taratibu za kuwasilisha Bajeti ya Manispa ya Musoma ya Mwaka 2013/14, Bajeti hiyo iliwasilishwa Wizara ya Fedha bila kukaa kwa kamati za Manispaa hiyo kisha kupitishwa kwenye Kikao cha Madiwani.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma Ahmed Sawa akisoma na kutolea ufafanuzi wa kina uliosaidia kumnasua Meya wa Manispaa hiyo Alex Kisurura kung'olewa kwenye madaraka yake, Mkurugenzi huyo alieleza kuwa waliamua kupeleka Bajeti ya Manispaa hiyo bila kupitia kwenye kamati husika kisha kwenye baraza la Madiwani ambapo madai yake makubwa yalikuwa ni kutokana na kubadilika kwa ratiba ya Bunge la bajeti ambalo litakaa Aprili mwaka huu badala ya Juni.
Nyie wote ni mabwana wadogo hamuwezi kuning'oa ng'o!
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Musoma Akitoa maelezo yake baada ya kuona ameelemewa na madiwani kuhusiana na habari kuwa amehusika kusaini na kupeleka Bajeti ya Manispaa hiyo bila kufuata taratibu za kupitia kwanza kwenye Kamati za Manispa kisha kwenye baraza la madiwani.
Na Thomas Dominick
Musoma
MEYA wa Manispaa ya Musoma Mkoa wa Mara Alex Kisurura (Chadema)
amenusurika katika mtego wa kung’olewa madarakani baada ya madiwani wa Manispaa
hiyo kuitisha Baraza la dharura ili kujua kwa nini Rasimu ya
Bajeti ya mwaka 2013/14 ilipelekwa hazina bila kufuata taratibu za
Manispaa hiyo inayoongozwa na Chadema.
Kikao hicho kilichokaa mwishoni mwa wiki kuanzia saa 8
mchana hadi saa 11 jioni kilikuwa mikakati hiyo ilianza hivi karibuni baada
ya kumtuhumu kuwa alishirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa Ahmed
Sawa kuwa wamepitisha na kusaini bajeti hiyo bila kufuata taratibu.
Mpango huo ulianza kuonekana baada ya wajumbe wa kamati
mbalimbali kugoma kwenda kwenye vikao vya kutipia bajeti wakidai kuwa
hawawezi kukaa hadi watakapoambia ni utaratibu gani umetumika
kupitisha bajeti hiyo.
“Bajeti yetu lazima iwe ya uwazi na ilitakiwa ijadiliwe na
kamati
mbalimbali kisha kuletwa kwenye kikao cha madiwani ili
tuweze
kuipitisha kisha kwenda wizarani, sasa tunataka kujua ni
taratibu gani zimepelekea bajeti hiyo kufika wizara ya fedha bila sisi
madiwani kuja? Alihoji Angela Derrick Diwani wa Kamnyonge.
Baada ya vuta nikuvute ya hapa na pale huku Mkurugenzi wa
Manispaa hiyo, Sawa alitoa maelezo ya kina kwa kusema kuwa Serikali
ilitoa maelekezo kuwa bajeti ya mwaka 2013/14 ilitakiwa
kuwasilishwa Wizara ya fedha haraka iwezekanavyo kabla ya Januari 31 mwaka huu.
“Baada ya kupokea barua kuwa inatakiwa bajeti ya mwaka
2013/14 na muda uliobakia ni mdogo ilibidi tufanye haraka kukimbizana na
muda na hii imetokana na mabadiliko ya kikao cha Bunge la bajeti ambalo
litakaa mwezi Aprili mwaka huu,”alisema Sawa.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa baada ya kuifikisha bajeti hiyo
wizarani waliiomba wizara ya fedha kuwa hiyo iliyopelekwa sio bajeti
kamili bali ni rasmu kutokana na kutopita kwenye kamati za Manispaa
husika na kuomba kuwa bajeti kamili itapelekwa baada ya kukaa na
kujadiliwa na kamati husika.
Alisema kuwa bajeti kamili inatakiwa kufikishwa hazina
Februari 20 mwaka huu ambapo mkurugenzi huyo aliitisha vikao vya kamati
mbalimbali lakini wajume wake
waligomea kuhudhuria vikao husika hadi watakapopata majibu ya kina.
Kutokana na maelezo marefu ya Mkurugenzi huyo madiwani
walianza kuhoji kuwa nani aliyesaini bajeti ambapo hapo ndipo walipokuwa
wanasubiria kuona kuwa Meya Kisurura kama amehusika kusaini ili mtego
wao wa kumtimua utimie.
Baada ya kuzungusha huku na kule ndipo Diwani Zeddy Sondobi akaamua kutoboa siri iliyojificha nyuma ya panzia kuwa ulikuwa
umetegwa mtego ambao kama angehusika kusaini bajeti hiyo ukomo wa Umeya
wake ungekuwa vumefika.
“Kwanza taarifa ya Meya ilikuwa inatuchanganya kuwa
halmashauri zingine zilikaa kabla ya bajeti hiyo kupelekwa wizarani na tukawa tunaulizana bajeti yetu imeendaje bila kusainiwa tukajua
lazima utakuwa umesaini na mtego wetu huu safari hii
usingeruka,”alisema Sondobi Diwani wa Bweri.
Baada ya kikao hicho mwandishi wa Blog hii alimtafuta mwenyekiti wa
Chadema Mkoa, Charles Kayele na kufanya naye mahojiano kuwa chama
hicho kilifanya kikao cha siri ili kujadili suala hilo na kufikia
maamuzi kuwa kama atakuwa ameshiriki kisiri kusaini bajeti hiyo
ataondolewa nafasi hiyo.
“Hatukufanya kikao chochote kile ndani ya chama lakini
tulikutana leo hii kabla ya kikao cha madiwani ambapo tulijadili sula hili
na
kumuuliza meya kama ameshiriki katika kusaini bajeti hiyo
ambapo
alikiri kuwa hakuusika na
wakati wa bajeti hiyo inaandaliwa alikuwa safirini Dar es salaam,”alisema Kayele.
Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA) Manispaa ya musoma
kimekuwa na mpasuko ndani ya chama hicho na migogoro ya hapa na pale
ambapo wakati wameingia katika uchaguzi wa naibu Meya madiwani hao waliafikiana nafasi hiyo wampatie diwani wa CCM, ambapo
mbunge wa jimbo hilo Vicent Nyerere aliingilia kati na kumaliza
tofauti hizo.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment