Askari wa kutuliza ghasia wa Mkoa wa Mara wakiwa katika eneo la tukio kuzuia ghasia kutoka kwa waendesha pikipiki na wananchi wa kijiji cha Etaro wilaya ya Butiama
Wananchi wa Kijiji cha Etaro wakiangalia nyumba ya Magee Saganda iliyochomwa moto baada ya mtoto wake Koti Magee kudaiwa kuhusika katika mauaji ya mwendesha pikipiki.
Baiskeli zikiwa zimeungua ndani ya nyumba ya mtuhumiwa wa mauaji ya kijana Magere Masatu.
wananchi wa Etaro wakishangaa tukio la uchomaji wa moto nyumba ya kijana anayetuhumiwa tukio la mauaji.
Na Thomas
Dominick,
Butiama
MAUAJI ya
kutisha bado yanaendelea kutokea katika Wilaya ya Butiama, Mkoa wa Mara baada
ya kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Magere Masatu Mkazi wa Mtaa wa
Nyakato, Wilaya ya Musoma kuuawa kasha kutupwa kwenye Mto wenye maji.
Katika
tukio hilo Wanajeshi waliingilia kati na walifanikiwa kudhibiti maafa zaidi
baada ya nyumba moja ya mtuhumiwa wa mauaji hayo kuchoma moto na kuteketeza
kila kitu.
Baadhi ya
mashuhuda wa tukio hilo wanadai kuwa tukio hilo lilitokea tarehe Februari 4
mwaka huu katika kijiji cha Etaro wilayani humo, ambapo walisema kuwa siku ya
tukio marehemu aligongana na pikipiki na mwenzake ambaye akufahamika jina lake.
Walisema
kuwa baada ya kugongana marehemu aliamua kumlipa fedha aliyegongana naye lakini
balozi wa eneo la tukio alipelekewa pikipiki ya marehemu kwa ajili ya
kuihifadhi.
“Baada ya
tukio kweli pikipiki ilichukuliwa na kupelekwa kwa balozi wakati wanakwenda
kuna vijana wawili walikuwa wakifuatilia kwa nyuma, na baada ya hapo marehemu
hakuonekana tena hadi jana alipoonekana amekufa na yupo ndani ya mto,”alisema
shuhuda aliyekataa kutaja jina lake.
Baada ya
waendesha pikipiki wa Wilaya ya Musoma kupata taarifa kwa kuuwa kwa mwenzao
walikwenda na kuvamia kijiji hicho kwa kuwapiga baadhi ya wananchi na balozi
ambaye alikuwa amehifadhi pikipiki hiyo kisha kumtaja mmoja wa wauaji hao kuwa
ni Koti Magee mkazi wa kijiji hicho.
Waendesha
pikipiki hao walikwenda hadi kwa mtuhumiwa huyo na walimkuta lakini alifanikiwa
kuwatoroka kisha kukimbilia ziwani na kujitosa kwenye maji kuogelea ikiwa ndio
pona yake.
Baada ya
kumkosa vijana hao walirudi nyumbani anapoishi kijana huyo ambaye anaishi na
baba yake mzazi aliyejulikana kwa jina la Magee Saganda kisha kuitia moto
nyumba moja na kuteketea kabisa.
Wanajeshi
wa Jeshi la wananchi waliwahi kufika katika eneo la tukio na kuzuia uchomaji
moto wa nyumba zingine ambazo nazo zilikuwa zinztaka kutiwa moto.
Mwandishi
wa habari alifika katika eneo la tukio ambapo kwenye nyumba hiyo hapakuwepo na
mtu yeyote yule lakini inadaiwa akina mama wa nyumba hiyo walipigwa na
waendesha pikipiki hao na kukimbilia kusikojulikana.
Jeshi la
polisi baada ya kufika lilichukua mwili wa marehemu na Balozi wa eneo hilo
Peter Mabojano na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho kwa ajili ya mahojiano
zaidi.
Mwili wa
marehemu umepelekwa katika Hospitali ya Mkoa huo na umehifadhiwa katika chumba
cha kuhifadhia maiti kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Tukio hili
ni la tano kutokea katika wilaya ya Butiama ambapo katika matukio ya kuanzia
Novemba mwaka jana hadi Februari mwaka huu ambapo matukio hayo ni kama
ifuatavyo
Matukio hayo ni pamoja na la Desemba 21, mwaka huu saa 5:30 usiku Tabu Makanya (68)
Mkazi wa Kijiji cha Kwikuba alichinjwa lakini watuhumiwa wakiwa katika harakati
ya kuondoka na kichwa chake waliwahiwa na wananchi kisha kukitupa.
Lingine lilitokea Desemba 2,Blandina Peru alichinjwa na kuchukuliwa damu yake tu na Sabina Mkireri
wa kijiji cha Kabegi, Kata alichinjwa na kuondoka na kichwa chake
Tukio
jingine ni la kijana aliyetambuliwa kwa jina la Thomas Majengo (23-28) Mkazi wa
Kiara Musoma Mjini alichijwa na kunyang'anywa pikipiki.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment